Na Mwandishi Wetu, TimesMajira,Online,Dar
WATU wanne kati yao watatu wakiwa ni askari wa Jeshi la Polisi
wamekufa katika tukio kubwa la kihalifu lililotokea jana mchana,
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na tukio hilo,
Kamishna wa P{olisi Oparesheni na Mafunzo, Lebaratus Sabas alisema
askari wakati wakiwa kazini alikuja mtu mmoja akaanza kuwashambulia
kwa silaha aina bastola.
Sabas alisema ya kuwashambulia askari hao na kuanguka alichukua silaha
mbili na kuanza kurusha risasi hovyo kuelekea Ubalozi wa Ufaransa.
“Alipofika eneo la ubalozi kuna kibanda, alianza kujihami kwenye
kibanda hicho, huku akiwa anafyatua risasi hovyo,” alisema Sabas na
kuongeza;
“Katika tukio hilo tumepoteza askari wetu watatu na mtumishi wa
kampuni ya ulinzi ya SGA.”
Aidha, Sabas alisema kuna watu wengine sita ambao ni majeruhi ambao
wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.
Aliahidi kuwa taarifa zaidi za tukio hilo zitaendelea kutolewa kadri
muda unavyozidi kwenda.
Aliongeza kwamba ni mapema sana kuweza kusema ni kwa nini mtu huyo
amefanya hivyo,lakini uchunguzi utabaini, kwani wameishaanzisha timu
ya upelelezi.
Aliwataka watu wengine wenye mahusiano na mtu huyo kujitokeza. Kuhusu
madai kwamba mtu huyo ni mkazi wa Upanga, Kamanda huyo alisema wao
hawafanyi upelelezi kupitia Vi-Clips, bali kwa kupitia upelelezi.
“Upelelezo ndio utakaosema huyo mtu ni wa Upanga sio Upanga, ni
Kinondoni kwa Manyanya au, Oysterbay, upelelezi utaonesha,” alisema
Kamanda.
Alipoulizwa kuna dalili zozote za ugaidi kwenye tukio hilo, Kamanda
alisema ni mapema, kwa hiyo uchunguzi ndiyo utakaosema au kuna tukio
la kawaida la mauaji.
Sabas alisema matukio kama hayo huwa yanatokea duniani, lakini
uchunguzi ndio utakaosema kama ni ugaidi au hakuna ugaidi.
Alipoulizwa kwamba mtu huyo anasemekana ni raia wa nchi za nje kamanda
huyo alijibu; “Hayo ni ya kwako sisi hatujasema, chuku ninachokisema
mimi, uchunguzi ndio utakaobaini, ni raia au sio raia, kama ni raia
anaishi wapi na lengo lilikuwa ni nini .”
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi