LONDON, England
NAHODHA wa timu ya Taifa ya England, Harry Kane anasema timu yao kupoteza kwa mikwaju ya penati kwenye fainali ya Euro 2020 dhidi ya Italia kutawatesa wachezaji katika maisha yao yote kwani ulikuwa “wakati mbaya zaidi kwake ulimwenguni”.
Katika mchezo huo, England ilikubali kichapo cha goli 3-2 kwa mikwaju ya penati, baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120, Marcus Rashford, Jadon Sancho na Bukayo Saka wote walikosa baada ya umaridadi wa Gianluigi Donnarumma kuziona penati zao.
England itaendeleza ukame bila kombe tena baada ya kushindwa kutumia fursa ya kuwa nyumbani; taji kubwa walibeba Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1966.
“penati ni hisia mbaya zaidi ulimwenguni wakati unapoteza. Haukuwa usiku wetu lakini tumekuwa na mashindano mazuri na tunapaswa kuendeleza hapo hapo.
“Kwa kweli itaumiza sana, Itauma kwa muda, lakini tuko kwenye njia sahihi na tunajenga na tunatumai tunaweza kuendeleza hapa mwaka ujao.
“Tunapaswa kujivunia sana kama timu kwa kile tulichofanikiwa. Sote ni washindi na tunataka kushinda kwa hiyo itaumiza kwa muda na itaumiza kwa kazi zetu zote, lakini huo ndio mpira wa miguu,” amesema Harry Kane
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania