January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Harry Kane ataka mataji Spurs

LONDON, England

MSHAMBULIAJI wa Tottenham Spurs, Harry Kane amesisitiza hamu yake ya kushinda mataji kufuatia kupoteza mchezo wao wa Fainali ya Kombe la Carabao akiwa na timu hiyo huku kukiwa na uvumi juu ya maisha yake ya baadaye .

Nahodha huyo wa England, bado hajatwaa kombe akiwa na Spurs, na kupoteza mbele ya Man City ni Mechi yake ya tatu Katika Fainali, “Msimu huu kama wa kukatisha tamaa. Ninataka kushinda mataji Makubwa zaidi na hapa bado hatufanyi hivyo kabisa,” amesema Kane.

Hata hivyo, Mkataba wa sasa wa Kane unaendelea hadi 2024, lakini amekuwa akihusishwa mara kwa mara kuondoka katika Siku za hivi karibuni huku akiwa ameifungia mabao 31 katika mechi 44 msimu huu na wiki hii alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu England.

“Tuzo binafsi ni nzuri na ni mafanikio mazuri. Ninapotazama nyuma mwishoni mwa kazi yangu, haya ndio mambo nitakayopita na kuchukua zaidi lakini lengo sasa hivi kama mchezaji ni kushinda mataji na timu. Ni uchungu kwamba, Ningependa kushinda mataji kwa timu hii lakini ndio sivyo,” amesema.

%%%%%%%%%%%%%