January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Harmonize kufanya Ziara Marekani

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Kondegang, Rajab Abdul maarufu kama’Harmonize’ anatarajia kufanya zira ya mziki nchini Marekani kuanzia Semptemba 3 hadi Oktoba 23 mwaka huu.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Harmonize amesema, ziara hiyo itaanzaia Semptemba 3 katika mji wa Hauston, Septemba 4-Ohio, Semptemba5-Minnessota, Septemba 18- Phoenix na Septemba 23 hadi 25 katika jiji la Las Vegas.

Harmonize amesema, ziara hiyo pia itafanyika mwezi Oktoba ambapo Oktomba mosi itafanyika New York, Oktoba 9- Los Angeles, Oktoba 16- Salt Lake City, Oktoba 22- Atlanta na Oktoba 23 itafanyika Syracuse, New York.