April 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hamburg,Dar watia saini hati ya makubaliano maeneo matano kushirikiana

Na Mwandishi wetu,timesmajira, Online

MJI waHamburg na Dar es Salaam umesaini hati ya makubaliano ya mashirikiano katika mambo matano yatakayosaidia jiji la Dar es Salaam kutengeneza ajira na kuongeza mapato.

Miongoni mwa maeneo hayo ni pamoja na Elimu,Afya,Ujasiriamali,kusaidia Wasanii pamoja na kupendezesha mji wa Dar es Salaam.

Akizungumza hayo leo jijini Dar es Salam ,Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Omary Kumbilamoto alisema mashirikiano hayo yaliyopo baina ya miji hiyo miwili yanatakiwa kudumishwa na kuendelezwa kwa sababu yanaleta umoja katika taifa.

Amesema kama viongozi wanaendelea kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kutangaza nchi kimataifa pia kujenga uchumi.

“Tunapowakaribisha wageni kuja nchini watakuja na fedha watazitumia katika mambo mbalimbali hiyo itatusaidia kuongeza mapato ya ndani na wafanyabiashara kufanya biashara na kujiongezea kipato,”amesema na kuongeza

“Haya ndo matendo ya Royal Tour imefanya wageni kuja na faids kubwa ni kupata mapato ya ndani kutokana na utalii,pato linakuja linaongezeka na linasaidia kutatua changamoto za wananchi, “amesema Meya Kumbilamoto

Amesema Rais Samia ameona utalii ni chanzo kipya cha kuongeza mapato katika nchi ,wageni wanakuja nchini na kufanya nchi kufunguka na kuongeza mapato.

Kwa Upande Afisa Mkazi Mji wa Hamburg jijini Dar es Salaam,Jinken Bruns amesema wataendeleza mashirikiano na jiji la Dar es Salaam katika mambo mbalimbali.

Amesema ushirikiano huo waliosaini jana utalenga katika sekta mbalimbali ambapo itasaidia kukuza uchumi na kuongeza mapato.

“Tunaadhimisha miaka 12 ya ushirikiano wetu baina ya Jiji la Dar es Salaam na Hamburg na urafiki huu utaendelea kuimarika siku zote katika kusaidiana mambo mbalimbali,”amesema

Naye Mwenyekiti wa wadau wa ushirikiano mji wa Dar es Salaam, Michael Onesmo amesema mahusiano hayo yatakwenda kuinua mapato ya jiji na kuongeza ajira hasa kwa vijana.

“Moja ya manufaa ya mahusiano haya kati ya jiji la Dar es Salaam na Hambury yatakwenda kuboresha uchuni wetu kwa kuongeza mapato ya jiji na kuongeza cha ajira,” amesema