November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Halmashauri ya Jiji yanunua Boti ya Doria

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamenunua boti ya doria ambayo itakuwa inafanya doria ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la feri.

Akizungumza na waandishi wa habari Meya wa Halmashauri ya Jiji OMARY KUMBILAMOTO alisema boti hiyo itafanya doria kwa ajili ya kudhibiti uvuvi haramu na kutunza Mazingira kwenye soko la samaki feri .

“Boti hii imenunuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Shilingi milioni 37 ambayo kazi yake kubwa kutatua changamoto sekta ya uvuvi hususani matukio ya uvuvi haramu ,utunzaji Mazingira na uokoaji watu ” alisema KUMBILAMOTO.

KUMBILAMOTO aliagiza boti hiyo ifanye kazi iliyokusudiwa isifanye kazi haramu hivyo naagiza Uongozi wa soko la feri isimamie ipasavyo na wakati wote iwe na mafuta Ili kuakikisha vitendo vya uvuvi haramu vinadhibitiwa .

Aidha alisema boti hiyo itakuwa chachu ya kuongeza ukusanyaji mapato kwa soko hilo na jiji kwa ujumla ,hivyo waitunze vizuri .

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharick Choughule amepongeza Serikali ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutekeleza ahadi yake ya Ununuzi wa boti ya kisasa ikiwa ni Moja ya kilio chake.

Diwani Sharick alisema ununuzi wa boti hiyo ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM walikuwa na kilio muda mrefu wa Ununuzi wa boti hiyo ambayo itafanya doria na uokoaji Kwa wavuvi kwenye mwalo.

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto (kulia)amezindua boti ya doria itakayotumika kukabiliana na wavuvi haramu Ufukwe wa Bahari ya Hindi Feri ,boti hiyo imenunuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa shilingi milioni 37 (kushoto )Diwani wa Kivukoni Sharick Choughule.