April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Gari alilotumia Rais Samia,Royal Tour lageuka kivutio Sabasaba

Na Mwandishi wetu Timesmajira

WANANCHI wanaotembelea katika Maonesho ya Biashara ya kimataifa ya 46 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es wamevutiwa na gari lilitotumiwa na Rais Samia Suluhu wakati wa uwaandaji wa filamu ya Royal Tour huku kila mmoja akitaka kupiga nalo picha.

Akizungumza jana na waandishi wa habari katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Felix John amesema gari hilo linaingia katika rekodi ya vivutio nchini kwakuwa lilitumiwa na Rais Samia na kuwavutia watu wengi.

Amesema wameamua kulileta gari hilo katika maonesho hayo ili wananchi walione mubashara na kupiga nalo picha.

“Gari hili linaingia katika rekodi ya vivutio vya kitalii si kwasababu tu kwamba lilitumiwa na Rais lakini pia aliliendesha kwa kuliheshimu kwa kumbeba Rais wakati uandaaji wa filamu ya Royal Tour ambayo imekwishaanza kuzaa matunda kutokana Watalii na wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuvutiwa kuja Tanzania kama sehemu ya Utalii na uwekezaji katika sekta mbalimbali.

“Kwakifupi matokeo chanya yashaonekana ikiwemo wingi wa Watalii ambapo hoteli zinafanya bisshara,bisshara mbalimbali zinafanyika na sekta ya usafiri wa anga ikiimarika kwakufanya bisshara ya usafirishaji abiria pamoja na mizigo “amesema John.

Kwa upande wake Kaimu Kamishna Msaidiza wa Uhifadhi Kituo Cha Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Dar es Salaam Hassan Nguluma amesema filamu hiyo imekuja kipindi muafaka kwakuwa Dunia ilikuwa ikipotoshwa kuhusiana na baadhi ya vivutio vilivyopo nchini kuwa vipo nchi jirani ilhali ukweli nikwamba viutio kama mlima Kilimanjaro Mbuga ya Serengeti vipo Tanzania lakini kwa Hila za kibiashara baadhi ya watu katika nchi jirani walikuwa wakinadi vivutio hivyo kuwa vipo nchini kwao.

“Hivyo basi kwa filamu hii imebatilisha uongo na uzishi uliokuwa ukisambazwa duniani kuwa vivutio hivyo vipo nchi jirani kitendo Cha Rais wa Nchi kushiriki kwenye filamu hiyo kumeijuza Dunia kuwa kweli vivutio hivyo vipo Tanzania na kwakuwa ni nchi ya amani na usalama umeimarishwa Watalii na wawekezaji wanakuja kwa wingi na uhakika wa usalama wao ukiwa ni kipaumbele namba Moja”amesema Nguluma