November 29, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Fyandomo achangia Mil.20 ujenzi nyumba ya Mapadri Rungwe

Na Mwandishi Wetu, TimesmajiraOnline,Rungwe

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Suma Fyandomo, amechangia Sh milioni 20 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya mapadri katika Kigango cha Watakatifu Petro na Paulo, kilichopo Tukuyu, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

Katika harambee hiyo iliyofanyika Nove28,2026, Fyandomo alikuwa mgeni rasmi, huku Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanjelwa, Askofu Gervas Nyaisonga, akizindua rasmi ujenzi wa jengo hilo na kulibariki.

Akizungumza katika hafla hiyo, Fyandomo amesema anatambua mchango mkubwa wa Kanisa Katoliki katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini, hususan uwekezaji wake katika vyuo mbalimbali vinavyowawezesha vijana kupata elimu na ujuzi.

Amesema katika harambee hiyo, kiasi cha Sh milioni 74 kilihitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo la ghorofa, ambapo Sh milioni 43 zilikuwa zimepatikana kupitia michango ya wadau, huku yeye akichangia Sh milioni 20.

“Tunatambua mchango mkubwa wa Kanisa Katoliki katika kushirikiana na Serikali kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo. Tutaendelea kuunga mkono juhudi za uwekezaji katika mradi huu ili kuhakikisha mapadri wetu wanapata mazingira mazuri ya kuishi na kutoa huduma bora kwa waumini,” amesema Fyandomo.

Kwa upande wake Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Mwanjelwa,Askofu Gervas Nyaisonga amewataka waumini kutumia ishara kujenga miundombinu ya nyumba za ibada na sio kuangalia rangi na uzuri pekee.

Nyaisonga amesema wanapoona msalaba wanaona picha ya Mungu ,lakini majengo mazuri ni ishara ya kuonyesha mwelekeo wa Mwenyezi Mungu.

“Wapo wanaokwazika wakiona ishara,lakini ishara uweke utulivu Mbele za Mungu kutokana uzao mteule wenye milki yake kumpa sifa,”amesema.

Nyaisonga amesema leo Jumamosi Novemba 28,2026 wakati akizundua jengo la maaskofu wa kanisa hilo na kuhimiza waumini kuwa na mfumo wa kujitokeza kuwekeza katika miundombinu ya kuabudu Mungu katika roho na kweli.

“Tusijenge majengo wakati roho zetu chafu na zina kutu bali tuliojenga kutambua wanapaswa kumwadumu Mungu kwa roho na kweli,lakini mmejitolea mwelezeni Mungu ili faida iwe ya roho sio kupata nini,”amesema.

Amesema hampendezi Mungu kuwekeza katika ujenzi wa nyumba za ibada huku mioyo ikiwa na kutu na ndio ufanya mengi na kukosa baraka za Mungu,huku akisisitiza Mungu anataka kuabudiwa katika roho na kweli lakini sio kulipa kitu.

“Wapo ambao wanatoa ,lakini wanaishi vibaya na wenzetu mnaweza kuchangia viti vizuri ,lakini Mungu apewi ibada ya roho na kweli pia yote ambaye mbafanya mjiulize namna mnavyoishi kwenye jamii na rohoni,”amesema.