May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

FEMA yatoa pongezi Kwa serikali kwa kuendelea kuwaunga mkono

Na David John timesmajira online Geita

KAMPUNI ya FEMA Mining and Drilling LTD inayojihusisha na uchimbaji,uchongaji na ulipuaji wa madini nchini iliyopo Munekeze-Katoro Mkoani Geita wameishukuru serikali kwa kutoa fursa na nafasi Kwa kampuni za kizawa kufanya kazi katika migodi iliyopo nchini.

Akizungumza katika maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita Mratibu mradi kutoka Kampuni FEMA MINING AND DRILLING LTD Mhandisi Jacquline Mtei amesema kuwa kwa sasa milango yakufanya kazi wazawa na kupewa kazi mbalimbali hasa kwenye sekta ya madini ni dhahiri kuwa sekta hiyo inazidi kukua siku hadi siku.

” Napenda kumshukuru Rais Dkt. Samia Hassan Suluhu kwa kuweza kutengeneza Mazingira ya uwezekano wa wazawa ‘makampuni mama’ kuweza kufanya kazi katika migodi yetu hii ya kati pamoja na Migodi mikubwa,Kupitia kampuni yetu ya FEMA sisi ni kampuni zawa kampuni ya kitanzania kwa hiyo tumeona mama alivyotengeneza mazingira ambayo imetuwezesha kapata zabuni katika migodi ya kati na mikubwa” Amesema Jacquline

Amesema kuwa Sekta ya madini inaoongoza kwakuchangia uchumi wa nchi hivyo inapotokea milango inapofunguliwa kwa wazawa kufanya kazi katika migodi hii pia itasaidia kukua zaidi kwani watatanguliza uzalendo katika nchi yao.

Aidha amewaaalika wanawake kusoma masomo ya sayansi hasa kuhusu miamba na madini kuwa wasiogope kazi zipo pia waondoe dhana potofu kuwa kazi zinazohusu madini ni wanaume pekee.

“fursa za ajira kwa wanawake katika sekta ya madini zipo sisi kampuni yetu imeweza kutusaidia sisi wanawake kupata ajira zaidi ya wanawake kumi na tano wamepata ajira nikiwemo mimi kwa hiyo wanawake wenzangu msiogope tuje huku”amewahasisha Jacquline

Kwa upande wake Afisa manunuzi na usambazaji kutoka FEMA Mining and Drilling LTD Frank Joseph amesema hao kama FEMA wameweza kushirikiana na makampuni tano tofauti katika kuwapa zabuni katika kampuni yao kama vile usambazaji wa vipuri,mafuta na virainisha kwa ajili ya mashine zao pia pamoja na huduma zingine ikiwemo usafi,chakula na huduma nyingine za kijamii.

Pia ameongeza kuwa katika katika kurudisha shukrani kwa jamiii kwa kile wanachokipata pia wameweza kusaidia kununua madawa katika zahati zinazo zunguka mgodi sanjari na kujenga shule na kukarabati vyumba vya madarasa ikiwemo kuzalisha ajira kwa vijana zaidi ya miamoja wanaozunguka mgodi.