Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Comrade Enock Koola, ambaye ni msomi wa masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Miradi, amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Hatua hiyo inaashiria dhamira yake ya kuchangia kikamilifu maendeleo ya wananchi wa Vunjo kupitia nafasi ya uwakilishi bungeni.
Mbali na taaluma yake, Enock Koola pia ni mfanyabiashara na mdau wa maendeleo ya jamii ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na jamii katika miradi ya kijamii na kiuchumi.
Kupitia uzoefu na maono yake, anaamini anaweza kuleta mabadiliko chanya na maendeleo endelevu kwa wananchi wa Jimbo la Vunjo.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi