May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Elimu ya ujuzi wa Tehama kuwanufaisha watu waliopo nje ya mfumo rasmi

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ambayo imewekeza sana katika miundombinu ya Tehama ambapo asilimia 94 ya maeneo yanayokaliwa na watu yamefikiwa na miundombinu ya mawasiliano Taasisi ya elimu ya watu Wazima kwa udhamini wa mfuko wa ujuzi wa mamlaka ya Elimu Tanzania ( TEA) wamekarabati karakana ya Compyuta ya Taasisi ya elimu ya watu Wazima.

Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa mradi wa kujumuisha kozi za TEHAMA katika programu ya IPOSA Chediel Mlavi amesema kuwa Karanakana ya kompyuta iliyokarabatiwa ina uwezo wa kubeba wanafunzi 20 na ina kompyuta 20 ambazo zote zimeunganishwa na huduma ya intaneti itatumika kutoa mafunzo kwa wanafunzi mbalimbali waliopo nje ya mfumo rasmi.

Amesema mradi huo ulikua na lengo la kuwapatia ujuzi watu mbalimbali waliopo nje ya mfumo rasmi ambapo wao walijikita katika kutoa ujuzi wa kompyuta kwa njia ya mtandao.

” Lengo kubwa la mradi ni kuwezesha taasisi na wananchi wa kitanzania kuweza kupata ujuzi kwa kutumia mtandao bila kukutana ana kwa ana ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza kama ilivyotokea kipindi cha COVID 19 ” amesema

Ameongeza kuwa mradi huo ulilenga kukarabati karakana ya TEHAMA ili kukamisha mafunzo ya njia ya mtandao yaliyojikita kwenye compyuta.

Kuhusu gharama za mradi huo amesema umegharimu kiasi cha shilingi milioni mia moja za kitanzania ambazo zilitolewa na mamlaka ya elimu Tanzania ( TEA) ambazo ziligawanyika katika mafungu mbalimbali huku akibainisha kuwa ukarabati wa karakana ya TEHAMA uligharimu shilingi milioni 11.

Kwa upande wake Mwanafunzi wa Taasisi ya elimu ya watu Wazima ambaye ni mnufaika wa mradi huo Aliuna Ferdinand amesema uwepo wa karakana hiyo utawasaidia wanafunzi kujifunza ujuzi wa kompyuta kwa njia ya mtandao.