Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Uyole Dkt. Tulia Ackson ametoboa siri kuhusu jina lake la ‘Mbozyo’ kuwa lilianzia kwenye kata ya Itezi baada ya kupewa na chifu wa kabila la Wasafwa.
Kwa tafsiri ya kabila la Wasafwa neno ‘Mbozyo’ lina maana ya dawa.
Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Uyole ambao waliamua kumchukulia fomu ya kuwania ubunge kwenye Jimbo hilo Dkt.Tulia amesema walichomfanyia wananchi hao ni mwendelezo wa heshima ambazo wamempa tangu awali.
“Wananchi wenzangu Sina cha kuwalipa, Mimi ni jirani yenu nina makazi yangu hapa, kwenye daftari mmeniorodhesha michango na kila kitu cha Maendeleo nitashiriki, ndio maana hata jina langu la ‘Mbozyo’ lilianzia hapa, chifu alipa hili jina nikiwa hapa uwanjani’ amesema Dk Tulia
Dkt.Tulia amewaambia wananchi wa Jimbo hilo kuwa ataendelea kushirikiana nao kuhakikisha kero na changamoto zao zinatatuliwa kwa haraka, kwani kiu yake kubwa ni kuhakikisha wanapata Maendeleo haraka.
Mwakilishi wa wananchi Justine Mwansepele amesema kiu ya wananchi wa Jimbo la Uyole ni kuona Dkt.Tulia Ackson ameridhia kugombea nafasi ya ubunge kwenye Jimbo hilo na kwamba wao wapo tayari kumpigia kura.
“Hatuna mashaka na Dkt.Tulia kwani tumeona kazi kubwa alizofanya kwa makundi mbalimbali kwani hakubagua kundi lolote akiwa Mbeya Mjini,sasa ni zamu ya Jimbo la Uyole”amesema Mwakilishi huyo wa Wananchi.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako