Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.Kellen-Rose Rwakatale amechukua rasmi fomu ya kugombea ubunge jimbo la Mlimba mkoani Morogoro.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Rwakatale amesema anayo dhamira ya dhati kulitumikia jimbo hilo la Mlimba kwani anazijua changamoto zake.
Rwakatale ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shule za St Mary’s ndani na nje ya Tanzania amerejea maneno ya wazee ambao pia walimuita hivi karibuni kumtia moyo agombee amesema hana mashaka kwani amechukua fomu na kura zitaamua vema.


More Stories
Mwenge waweka jiwe la msingi madarasa matatu Tunduma
Bunge lipo tayari kushirikiana na Mabunge mengine
TADB yatoa tuzo kwa wanafunzi 13 SUA