January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt Philip Mpango kufungua kongamano la 14 la kisayansi Arusha

Na Queen Lema, Timesmajira Online,Arusha

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philiph Mpango anatarajiwa kufungua kongamono la 14 la kisayansi ambalo litaaanza jijini Arusha Desemba 6,mwaka huu.

Akizungumza na waandishi habari jijini Arusha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania(TAWIRI)Dkt.Ernest Mjingo amesema kuwa kongamono hilo litafanyika kwa siku 3.

Ameeleza kuwa mpaka sasa zaidi ya washiriki 300 wamesha thibitisha ushiriki wao huku nchi zaidi ya 22 nazo zimeweza kuthibitisha kushiriki katika kongamano hilo ambalo pia ni fursa ya utalii kwa Tanzania.

Pia amesema kuwa TAWIRI ni moja ya taasisi ambayo jukumu lake ni kufanya tafiti mbalimbali juu ya wanyamapori lakini pia inatoa taarifa sahihi kwa wakati hivyo basi ndani ya kongamano hilo wataweza kujadili mambo mbalimbali ikiwemo tafiti.

“Kama ambavyo wote tunajua na kutambua kuwa tafiti ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki ndani ya kongamano hilo ambalo Mgeni wetu wa Heshima ni Makamu wa Rais tutazungumzia tafiti lakini pia tutakuwa na mada nyingine ambazo nazo zinalenga kwenye sekta ya utalii,”ameongeza.

Aidha ametaja mada ambayo itaongozwa na kongamano hilo kuwa ni pamoja na mada ya mgongano baina ya binadamu na wanyamapori.

Mada nyingine ambazo zitajadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na mimea vamizi ndani ya baadhi ya hifadhi ambapo mimea hiyo imeonekana kuchukua sehemu kubwa ya malisho ya wanyamapori.

Sanjari na hayo amewataka wadau wa utalii,wananchi,watafiti kuhakikisha kuwa wanajumuika pamoja kwenye mkutano huo ambao utaweza kuleta mabadiliko kwenye sekta ya utalii.