Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online-Njombe
Vitongoji 125, vikivyopo katika Jimbo la Ludewa vimeahidiwa kufikishiwa nishati ya umeme endapo Chama Cha Mapindizi(CCM), kitapata ridhaa kwa .ara nyingine ya kushika dola katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.
Ahadi hiyo imetolewa Septemba 22,2025, na mgombea mwenza wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Halmashauri ya Ludewa, uliopo kwenye eneo la Bomani mkoani Njombe.

Ambapo ameendelea kukinadi chama hicho na kumuombea kura za ndiyo, Rasi Dkt. Samia Suluhu Hassangombea Ubunge wa Jimbo la Ludewa, Joseph Kamonga na madiwani.wa CCM.
Amesema, katika kipindi cha miaka mitano ijayo, mbali na vitongoji hivyo kupata umeme, pia kuna muradi mingine ya maendeleo watakayo nufaika nayo wananchi hao, kuwa ni pamoja na uboreshwaji wa huduma za afya, ikiwemo hospitali ya wilaya, kujenga vituo vya afya 14 na zahanati nane.
Pia kujenga shule za msingi tano,sekondari sita, maaabara 12, mabweni ya wanafunzi wa kike 14 na upanuzi wa shule za zamani kwa kuongeza madarasa 344.
Dkt.Nchimbi,amesema,upo mpango wa kuboresha miundombinu ya barabara kwa kiwango la lami na changarawe jimboni humo ikiwemo ujenzi wa madaraja.
Aidha Dkt. Nchimbi amesema, kutokana na asilimia kubwa ya wananchi wa Ludewa kujihusisisha na shughuli za Kilimo, Serikali itahakikisha inaimarisha utaratibu wa utolewaji wa mbolea na mbegu za ruzuku na ujenzi wa maghala sita ya kuhifadhia mazao.

Sanjari na kutoa mashine tano za kubangulia korosho na mashine tano za kuchakata kahawa pamoja na upanuzi wa mradi wa umwagiliaji hususani katika eneo la Mchuchuma,pia kujenga maeneo matano ya kuogeshea mifugo ‘Majosho’ na machinjio mawili ya kisasa.
Kwa upande wake mgombea Ubunge wa Jimbo la Ludewa kupitia CCM, Joseph Kamonga, amesema akipata ridhaa ya kuwa Mbunge, atakahikisha miradi ya maendeleo inaendelea kufika kwa wingi jimboni humo.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI