December 31, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Kijaji aridhishwa na Kongani ya Viwanda (SINO TAN] Kwala

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan inaunga mkono jitihada zinazofanywa na wawekezaji katika kusaidia juhudi za uzalishaji na upatikanaji ajira kutokana na viwanda na uwekezaji nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa,
Viwanda na Biashara Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji  Novemba 30, 2023 alipotembelea Kongani ya Viwanda (SINO TAN] Kwala wilayani kibaha kuangalia maendeleo ya uwekezaji unaoendelea ambao mpaka sasa umekamilisha viwanda 2 nje ya zaidi ya viwanda 250 vya kuchakata malighafi na kutengeneza bidhaa ikiiwemo mavazi ndani ya mwaka huu 2023 na kuongezeka kwa uwekezaji na nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania zaidi ya laki 2.

’Nimetembelea viwanda viwili kati ya 250 na kimoja wapo ni cha nguo [vijora] na taarifa njema nimeambiwa bidhaa zinazotengenezwa zinatumika ndani ya Tanzania na vinasambazwa Dubai pamoja na Zambia nimefurahishwa sana ni hivyo ni wazi taifa letu limeanza kupata fedha za kigeni kutokana na uwekezaji unaoendelea. Amesema Dkt. Kijaji

‘Leo nimekutana na wawekezaji wa Hunan Pia wao wanatazama namna ya kuwekeza hapa na nimpögeze Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kutufungulia Milango ya wawekezaji nchini’ Ameongeza Dkt. Kijaji.

Aidha ameeleza kuwa ajira zimetengenezwa kwa ukubwa asilimia 90 ya mabinti waliopata ajira wanatoka kwala.

Aidha amesema ameridhishwa naridhishwa na kasi ya utekelezaji wa yale niliyoagiza mwezi wa 8 na tutegemee ajira zaidi hapa SINO TAN kibaha na changamoto ya kutopata feda za kigeni litatatuliwa na uwekezaji huu hapa na kila kijana uchumi wake utabadilika.