Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WIZARA ya Madini imetaja mafanikio lukuki katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani Machi 19 mwaka jana ikiwemo katika suala zima la sekta hiyo kuchangia katika pato la Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Dotto Biteko alisema,chini ya uongozi wa Sertikali ya awamu ya Sita ,mchango wa sekta ya Madini katika pato la Taifa umekuwa ukiongezeka kutoka robo moja ya mwaka hadi nyingine katika kipindi cha Januari –Septemba 2021 wastani wa sekta hiyo umekua hadi kufikia asilimia 7.3 ya pato la Taifa ikilinganishwa na wastani wa asilimia 6.5 katika kipindi kama hiki cha mwaka 2020.
Dkt.Biteko alisema,katika robo ya tatu Julai –Septemba 2021 mchango wa sekta ya madini uliongezeka hadi kufikia asilimia 7.9 ya pato la Taifa kutoka asilimia 7.3 ya pato la Taifa katika kipindi kama hiki mwaka 2020.
“Matokeo haya yanaakisi dhamira ya Serikali kuhakikisha sekta hii inaimarika na kuweza kuchangia pato la Taifa asilimia 10 ifikapo mwaka 2025 kama ilivyotangazwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa na Mpango wa Maendeleo .”alisema Dkt.Biteko na kuongeza kuwa
“Kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya awamu ya sita sekya ya madini imeweka historia kwa kushuhudia mauzo ya moja kwa moja yenye thamani ya shilingi trilioni 8.3 kutokana na mauzo ya madini ya aina mbalimbali yakiwemo ya Dhahabu,Fedha,Shaba,Makaa ya Mawe,Kinywe ,Vito na madini ya Ujenzi wa Viwanda.”
Alisema kutokana na biashara ya madini hayo wizara imekusanya shilingi bilioni 597.53 kama maduhuli ya Serikali yaliyokusanywa kupitia Wizara hiyo ambapo ushiriki wa watanzania kwenye shughuli za madini umekua kutoka asilimia 48 hadi asilimia 63 na hivyo kuongeza thamni ya huduma migodini kufikia thamani ya Dola za Marekani 579.3 sawa na shilingi Trilioni 1.33 kutokana na huduma zilizotolewa migodini.
Aidha Dkt.Biteko alisema wizara hiyo imeongeza usimamizi kwenye madini ya ujenzi,viwandani ambapo tayari mifumo ya kielektroniki imeanza kutumika katika usimamizi wa mapato ya serikali yatokanayo na madini hayo.
Alisema katika kusimamia upatikanaji wa mapato kutokana na madini ya ujenzi na viwandani Wizara ya Madini imeanzaushirikiano na wizara ya Tamisemi ili kuweza kuwafikia wananchi wanaotumia madini hayo waweze kuchangia fedha zitokanazo na shughuliza uchimbaji madini hjayo kwa majibu wa sheria ya madini.
Mikataba
Kuhusu eneo hilo alisema katrika historia ya sekta ya madini imefanikiwa kusaini mikataba mipya mine ya uchimbaji na uanzishwaji wa migodi mikubwa nay a kati ya madini kwa wakati mmoja .
“Disemba 13 ,2021 Dunia ilishuhudia Serikali ya Mheshimiwa Rais Samia na yeye mwenyewe akiwepo kwenye tukio hilo ikisaini mikataba ya uwekezaji wenye thamani ya dola za Marekani milioni 735.79 ,mikataba hiyo ilihusisha uchimbaji wa madini muhimu ya viwandani yanayotokana na mchanga wa baharini,madini ya Dhahabu ,Almasi na Madini ya Kinywe(Graphite).
“Matokeo na mafanikio hayo yanatokana na jitihada mbalimbali za Serikali ya awamu ya Sita ikiwa ni pamoja na kuimarisha taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini .”alisema Dkt.Biteko
Tozo
Kuhusu tozo katika sekta hiyo alisema juhudi mbalimbali zimefanyika katika awamu ya sita za kupunguza adha za tozo zisizokuwa na tija kwa wananchi na wawekezaji katika sekta ya madini ambapo marekebisho yamefanyika katika sheria ya Madini Sura 123 kwa vipengele ambavyo vilikuwa vinaleta mkwamo katika ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali.
“Tume ya Madini sasa inatoa leseni ndogo za biashara ya amadini ya ujenzi nay a viwandani ambayo yatachochea na kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye uchimbaji na biashara ya madini hayo na hivyo kuongeza wigo wa ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali kupitia madini ujenzi na viwandani.”
Taasisi ya jiolojia n utafiti wa Madini(GST)
Katika eneo hilo Dkt.Biteko alisema,katika kuhakikisha inatimiza malengo yake ipasavyo ,imefanikiwa kusogeza karibu na wachimbaji wadogo wa madini huduma za maabra kwa lengo la kuwasaidia wachimbe kisayansi na hivyo kuongeza tija na mapato ya Serikali .
More Stories
Mwinyi: Kuna ongezeko la wawekezaji Zanzibar
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Maofisa Watendaji watakiwa kufanya kazi kwa weledi