Judith Ferdinand , Timesmajira Online -Mwanza
Dirisha la uchukuaji fomu za kuwania nafasi za Ubunge na Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) limefunguliwa rasmi Juni 28,2025 na linatarajia kufungwa Julai 2,2025.
Ambapo Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula,amekuwa mtia nia wa kwanza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo hilo kupitia CCM,akitetea kiti hicho kwa mara ya tatu.
Dkt.Angeline mbali na Ubunge pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini na kwenye chama ikiwemo Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilemela,Naibu Waziri na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.Pia amewahi kuacha kazi ili aweze kupata fursa ya kuwatumiakia wananchi.
Kada mwingine alichukua fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Ilemela ni Leonard Qwihaya maarufu Manguzo,Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Ikiwa ni mara ya kwanza kuchukua fomu na kuwania nafasi hiyo.
Wote wawili walikabidbiwa fomu na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela, Hassan Millanga Juni 28,2025 katika ofisi ya chama hicho ngazi ya wilaya.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomi Dkt Angeline,amesema hana wasiwasi kutokana na kazi nzuri alizofanya jimboni Ilemela huku Leonard,ameeleza sababu ya kuamua kuchukua fomu na kutia nia ya kugombea nafasi ya Ubunge ni kutaka kuwatumikia wana Ilemela.
Tumaini la wanachama wa CCM na wakazi wa Ilemela,la yupi atapeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya Ubunge jimboni Ilemela lipo katika kura za maoni za chama hicho.
Mbali na hao,Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Khadija Liganga ‘Dida’ anayewakilisha Mkoa wa Mwanza, pamoja na Halima Nassor, Kada wa CCM,wamechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge wa viti maalum kwa kundi la wanawake.
Dida pia ni muandaaji wa tuzo maarufu za Mwanamke Kinara zinazotolewa kwa wanawake wa Kanda ya Ziwa wanaofanya vizuri katika sekta mbalimbali.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako