May 4, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Angeline atangaza neema kwa Wanakitangiri

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Ilemela Dkt. Angeline Mabula kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amewahaidi wananchi wa Kata ya Kitangiri Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kutatua changamoto zilizopo ikiwemo barabara, elimu, uvuvi na maji pamoja na kuwaletea maendeleo zaidi endapo watachagua Rais, Mbunge na Diwani anatetokana na chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni zinazoendelea uliofanyika kwenye uwanja wa Mihama Kata ya Kitangiri, Dkt.Angeline amesema, milioni 64 zimetengwa kwa ajili mambo yafuatayo ikiwemo ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya Mihama ambayo imetengwa milioni 10, milioni 15 shule ya Mwinuko sekondari pia milioni 30 hapo hapo Mwinuko kwa ajili ya ujenzi wa maabara.

Amesema hayo yote yatafanikiwa endapo watamchagua yeye na mgombe udiwani wa kata hiyo ambaye kitu cha kwanza baada ya uchaguzi anapaswa kuzipigia kelele fedha hizo ili mambo hayo yaweze kufanyika kwani zinatokana na mapato ya ndani.

Dkt. Angeline amesema kuwa, anatambua eneo la Mihama ni la wavuvi wengi wanaoishi, hivyo zimetengwa milioni 250 kwa ajili ya kuboresha mialo ya Mihama, Kayenze na Igombe kwani wanatambua mialo hiyo ndiko haswa mazao ya samaki yanapatikana na mnatambua kwa juhudi za jemedari Dkt.Magufuli uwanja wetu wa ndege unatanuliwa na ndege kubwa zinatua pale pia zimetengwa milioni 50 kwa ajili ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ndani ya Ziwa na watakaonufaika ni wananchi wa Ilemela waliopo katika mialo hiyo.

Meneja Kampeni wa CCM Jimbo la Ilemela Kazungu Idebe (kushoto) akimnadi mgombea Ubunge Jimbo hilo kupitia chama hicho Dkt.Angeline Mabula katika mkutano wa kampeni wa kuomba kura kwa wananchi uliyofanyika uwanja wa Mihama Kata ya Kitangiri. (Picha na Judith Ferdinand).

“Mlimsikia juzi akisema mazao ya samaki yanapelekwa moja kwa moja Ulaya na hayapitii tena nchi ya jirani,haziwezi kutua hapa kama hatuna mialo yenye kiwango kinachokubalika,ubora unao takiwa na mazao ya samaki yanapatikana ndio maana mwalo huu wa Mihama ni mmoja unaenda kutengeneza na kukarabati vizuri ili uweze kuvuna mazao ya samaki na kuweza kutoka yaende kiwandani na hatimaye nje ya nchi bila usumbufu na kutegemea nchi jirani,”amesema Dkt.Angeline.

Pia amesema,baada ya kumpa kura zote atashirikiana na mgombea udiwani huyo kufanyia kazi mapungufu ya barabara hiyo ya Mihama na kuhakikisha inatengenezwa na kazi itaanza mara tu watakapokuwa wameingia madarakani hivyo watakazo buti kuhakikisha zahanati au kituo cha afya kinapatikana katika kata yao.

Hata hivyo amesema, pia wanasimamia kuhakisha watu wote wanapata umeme kwani wakati anaingia madarakani asilimia 35 ya watu wa Jimbo zima ndio walikuwa wanapata umeme ila sasa ni asilimia 75 kwaio wamebakiza asilimia 25 hivyo anawaomba hawajafikiwa wawe na amani umeme utawafikia.

Aidha amesema kuwa, kero ya ukosefu wa maji imeanza kuacha kuwa kitendawili kwa sababu mitego yote imeanza kuteguliwa,kama jambo ambalo walilokuwa wanalivalia njunga ni sekta ya maji ambapo wanajua maji ni uhai na bila maji mambo hayaendi na kwenye taasisi wamepeleka maji na tenki limeisha jengwa na kinachifuata ni kusambazwa maji.

“Maji yatasambazwa kwa kila nyumba kwa kila muhitaji na kwa wale ambao hawana uwezo Serikali ya Dkt.JohnMagufuli imeisha ridhia watoe 21,000,naomba hili tusilijumuishe tofauti ni kwa wale wasiokuwa na uwezo,maana kila mmoja akiwekewa kwa bei hiyo hata MWAUWASA itajikuta inashindwa kufanya kazi na kushindwa kutimiza malengo yao,” amesema Dkt. Angeline.

Kwa upande wake Meneja Kampeni wa CCM Jimbo la Ilemela Kazungu Idebe amesema mgombea Ubunge huyo baada ya kuingia madarakani awamu ya kwanza alianza na vipaumbele ambavyo alikuwa ameviweka na alivyokuwa ameendelea kwahaidi ikiwemo kuboresha suala la elimu na miundombinu yake katika jimbo hilo ambapo tayari zinekuwepo shule mpya tatu za msingi na tatu za sekondari katika kipindi cha miaka mitano.

“Katika mtindo huo huo wa utatu mtakatifu kwa maana ya wa wananchi nyie mnaanzisha yeye anaweka juhudi kubwa zaidi na Halmashauri ikikamilusha ameendelea kufanya mambo makubwa tumejenga vyumba vipya vya madarasa 89,kulikuwa na changamoto ya Mihama na Mwinuko kila shule ilipatiwa milioni moja moja kwa ajili ya moja ipate maji na nyingine umeme ili watoto wasome vizuri,”amesema Kazungu.