Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali inaweka mifumo bora kwa ajili ya kuboresha kazi za sanaa na kulinda masalahi ya wasanii.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo Mei 9, 2021 kwenye Iftar maalum iliyoandaliwa na Star Times kuzindua tamthilia mpya ya WE-MEN na Chaneli mpya ya TV3 katika Ukumbi wa Hyatti jijini Dar es salaam.
“Kazi za Wasanii wengi wa hapa nchini zinachezwa na kuangaliwa sana duniani lakini wamiliki wa kazi hizo hampati chochote” amesema Dkt. Abbasi.
Dkt. Abbasi amefafanua kuwa kupitia mwaka mpya wa fedha wa 2021/22 Serikali itakua na kodi maalumu ya kutoza makampuni mbalimbali yanayokuja nchini kwa ajili ya kutumia ama kuuza kazi za wasanii ambayo itamfaidisha msanii moja kwa moja.
Aidha Katibu Mkuu Dkt.Abbasi amewasisitiza wasanii kufanya kazi bora kwasabau muziki, filamu na sanaa zima kwa ujumla duniani ipo katika ushindani mkubwa, hivyo wanapaswa kutengeneza kazi zenye kiwango cha hali ya juu kukidhi mahitaji na Soko Duniani.
Hata hivyo Dkt. Abbasi ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuwekeza katika filamu za kitanzania na pia kwa kuanzisha Chaneli mpya ya TV3 itakayokuwa inarusha mashindano ya EURO 2020 ambayo uchambuzi wa mashindano hayo utakuwa ukifanyika kwa lugha ya kiswahili.
“Nawashukuru Star Times kwa kazi kubwa mnayoifanya Tanzania, mmetafuta soko la kazi zetu za sanaa hongereni sana” Dkt. Abbasi.
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo