Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Diwani wa Kata ya Kitunda Victor Vedasto, amezindua kampeni ya kupanda miti kata ya Kitunda katika juhudi za kuunga mkono Serikali suala la utunzaji Mazingira.
Diwani Victor Vedasto, alizindua kampeni hiyo kwa kupanda miti katika za msingi na sekondari zilizopo Kata hiyo kwa kushirikiana na wadau wa Mazingira taasisi tatu zosizo za Serikali Help the child the Youth &women Tanzania Foundation ,Tuinuke woman Development Organization(TUWODO )na Budeo Buguruni Development Organization ambazo zinaisaidia Serikali sekta ya Mazingira.
Akizungumza katika uzinduzi huo Diwani Victor Vedasto, alisema mwaka huu 2024 Kitunda wanatarajia kupanda miti 500 katika taasisi za Serikali shule na katika makazi ya wananchi .
“Ninawapongeza hizi taasisi zisizo za Serikali kampeni yao hii ya utunzaji mazingira Kitunda tunatarajia kupanda miti 500 ninawaomba wananchi wangu tushirikiane na Serikali kila kaya ipande miti mitano ya matunda na vivuli ili Kitunda yetu iweze kuwa ya kijani” alisema Vedasto.
Alisema taasisi tatu zimeungana katika mabadiliko ya tabia ya nchi katika suala la Mazingira kupanda miti na kutoa elimu kwa wanafunzi ili waweze kuwa mabalozi wa Mazingira.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali Tuinuke Woman Development Organization (TUWODO)Awena Omary alisema kampeni ya upandaji miti wanatarajia kupanda miti 1500 katika kuisaidia Serikali kutunza mazingira katika mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mkurugenzi Awena Omary, alisema kampeni hiyo ya kupanda miti ni endelevu kata saba za wilaya ya Ilala ambazo ni Kata ya Kitunda ,kata ya Kipawa,Kata ya Kiwalani, Vingunguti, Mnyamani, Buguruni, na Minazi Mirefu .
Awena alisema miti hiyo ya matunda na vivuli wamepewa na TFS wilaya ya Ilala ambapo kata ya Kitunda walipanda shule ya Makala Mengi Sekondari, Kitunda Sekondari, Jitihada shule ya msingi Kipera Shule ya Msingi.
Mkurugenzi Awena Omary alitumia fursa hiyo kutoa elimu ya utunzaji mazingira kwa wanafunzi wa Kitunda ili wawe mabalozi wazuri watunze miti hiyo mpaka ikue mikubwa.
Mkurugenzi wa Help the Child ,the Youth &Women Tz foundation Agines Kituta alisema lengo la kupanda miti hiyo Ilala iwe ya kijani kwani ni muhimu kwa ajili ya kutunza hali ya hewa na vyanzo vya maji .
Agines Kituta alitumia fursa hiyo kuwashukuru TFS kwa kuwapatia miti hiyo ambayo inapandwa katika shule za Serikali zilizopo Wilayani Ilala.
Mkurugenzi wa Budeo Buguruni Development Organization Khamsini omari alisema shirika la Budeo sio la kiserikali linajishugulisha na shughuli za kijamii katika kuisaidia Serikali ambapo kampeni hiyo ya kupanda miti ni endelevu kila mwaka mashirika hayo yanajiujinga pamoja na Serikali katika upandaji huo .
More Stories
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto
Kilo 673.2,dawa za kulevya zakamatwa Bahari ya Hindi