BARCELONA, Uhispania
NYOTA wa klabu ya Barcelona, Frenkie de Jong amesema bado ataendelea kusalia katika klabu hiyo ili kutimiza malengo yake licha ya Man United kumuhitaji.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alihusishwa na kuhamia Old Trafford wakati wote wa majira ya joto huku kukiwa na mzozo wa kutolipwa mshahara huko Barca, lakini akaishia kusalia Uhispania licha ya juhudi kubwa za United kufanya mazungumzo ya makubaliano.
De Jong hapo awali alifanya kazi chini ya meneja wa sasa wa United Erik ten Hag huko Ajax na anajulikana kuwa bado anawasiliana na meneja wake wa zamani.
Kwa mujibu wa mtandao wa dakika 90, unaelewa kuwa United badi inavutiwa na De Jong kwenda Manchester, huku wakitafuta kujiimarisha tena kama nguvu kubwa katika soka la Ulaya, lakini hakuna mwelekeo kwamba kiungo huyo wa kati wa Uholanzi atataka kulazimisha kuondoka Catalonia.
Hata hivyo, De Jong ameonesha kwamba anataka kubaki Barcelona kwa sasa na kuendelea kutimiza ndoto yake ya utotoni.
“Nilikuwa mtulivu, kwa sababu nilijua nilitaka kuendelea na Barca na sijabadilisha maoni yangu,” amesema De Jong.
“Siku zote nilikuwa na ndoto ya kuichezea Barca na ninataka kufanikiwa kama mchezaji wa Barca. Na sasa nimetulia na nataka kuendelea Barca,” ameongeza.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025