January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Masalla: Mazoezi ni njia ya kupambana na UVIKO 19

Judith Ferdinandtimesmajira,Mwanza

MKUU wa Wilaya Ilemela Hassan Masalla,amesema mazoezi ni afya,mshikamano,yanajenga uhusiano,ushirikiano na kuleta maendeleo pamoja na njia ya kupambana na maradhi ikiwemo UVIKO-19.

Hivyo amewaomba wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujijenga,kuimarisha afya na kupiga vita kuenea kwa maambukizi ya UVIKO-19.

 Masalla amesema hayo jana,wakati akizindua rasmi kikundi cha mchezo wa mbio za kawaida(jogging club) pamoja na mazoezi ya viungo vya mwili kwa wananchi wa Wilaya ya Ilemela,uliofanyika katika uwanja wa Sabasaba.

 Mkuu huyo wa Wilaya,viongozi mbalimbali wa serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi walipata fursa ya kukimbia umbali wa km 8.2,kufanya mazoezi ya viungo sanjari na kupima afya zao pia kulikuwa na fursa ya utoaji chanjo ya UVIKO-19.

Akizungumza mara baada ya kuzindua  mbio hizo,Massala amesema anatambua  mazoezi ni afya ,umoja na mshikamano na yanajenga uhusiano yatakayoleta ushirikiano utakaosaidia kuleta maendeleo .

“Mimi nimeanza mazoezi nikiwa na umri mdogo wa miaka saba mpaka sasa nafanya ukiniangalia afya yangu ipo vizuri leo kupitia mazoezi haya nimepata marafiki wapya ambao tutajenga ushirikiano na kupiga hatua,”amesema

Kwa upande wake Ofisa Michezo wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Kizito Bahati, amesema watakuwa wanakutana mara moja kwa mwezi ambapo itakuwa wiki ya pili kwa kila mwezi.

Katibu wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) ,Aron Mikonangwa  Nyamilonda lll amesema mazoezi yanasaidia kurudisha umri nyuma kwa sababu yanaujenga mwili  ipasavyo na kupambana na magonjwa mbalimbali ikiwa yeye anaumri wa miaka 60 lakini angalia akionekana kijana.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ilemela (OCD) Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Elisante Ulomi amesema, mazoezi yanapunguza vitendo ya uhalifu hiyo ni mara baada vijana kujiunga na vikundi vya mazoezi, mawazo ya kufanya matukio mabaya wanakosa muda ya kutenda hivyo alitoa hamasa kwa vijana kujiunga kwenye vikundi vya mazoezi ili kuondokana na uhalifu.