Na Heri Shaaban
MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija amewapa kibano Mafundi waliopewa tenda ya ujenzi wa madarasa ya Shule za Sekondari yanayojengwa kwa fedha kutoka Shirika la Fedha la kimataifa IMF akiwataka ujenzi wa Madarasa hayo ujengwe kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya Ludigija alitoa tamko hilo leo katika ziara yake na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kukagua maendeleo ya madarasa hayo ambayo yanatakiwa yakamilike mwezi Desemba mwaka huu.
“Wakandarasi wote ambao wamepewa tenda katika ujenzi wa shule hizi wapewe fedha zao watumie wafanyakazi wa kutosha madarasa yamalizike kwa haraka ili watoto wetu waweze kusoma January “alisema Ludigija
Katika ziara hiyo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya wametembelea shule za sekondari za Jimbo la Ilala ,Jimbo la Segerea na Jimbo la Ukonga ambapo kote serikali imepeleka fedha kila kata kwa ajili ya madarasa ili Mwezi January wanafunzi wa kidato cha kwanza wasome
Ludigija alisema jumla ya madarasa 255 ya Sekondari yatarajia kujengwa Wilaya ya Ilala kufuatia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwapatia fedha shilingi bilioni 5.1ambazo zitajenga madarasa 255
“Nampongeza Rais wetu kuwekeza katika sekta ya Elimu ametupatia fedha za kutosha shilingi Bilioni 5.1 kwa ajili ya ujenzi vyumba vya madarasa ujenzi unaendelea vizuri tutasimamia fedha hizi kufanikisha ujenzi wa madarasa 255 “alisema Ludigija
Alisema ziara hiyo ni endelevu kukagua madarasa ya shule za zote za Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam lenye shule 41 jana amefanikiwa kukagua shule nane kati 41 Msimbazi ,Mchikichini na Mivinjeni,Jimbo la Ilala ,Segerea wamekagua kuangalia maendeleo ya ujenzi shule za Magoza Kisukuru na Bonyokwa pamoja na Jimbo la Ukonga .
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti