May 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Bulembo atishia kuwaondoa kazini watumishi wasio waadilifu

Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Muheza

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Halima Bulembo amewatishia kuwaondoa kazini watendaji watakaofanya mchezo na shilingi milioni 180 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwajili ya ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023.

Kauli hiyo ameitoa kwenye kikao cha kwanza cha robo ya kwanza cha baraza la madiwani katika mwaka wa fedha 2022/2023 katika Halmashauri ya wilaya ya Muheza.

Bulembo ametoa angalizo juu ya matumizi ya kiasi cha shilingi milioni 180 fedha zilizotolewa na Rais kwajili ya ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa.

“Huwezi kazi utasaidiwa yaani hatutogombana na mtu watu wanaotafuta kazi ni wengi sana kwahiyo kama kazi yako imeshakuwa ni mazoea unaweza kufanya unavyotaka tutakuja na tutakuambia kaa pembeni tutampa yule anayetaka hiyo kazi akusaidie huo ndio utaratibu wala hatutoshemeshana,”alisititiza Bulembo.

“Ili tusifike huko mnaohusika mkasimamie inavyotakiwa tarehe 30 ndio dead line yangu mimi na viomgozi wa wilaya tutapokea hayo madarasa na tarehe 15 tutakuwa tunasubiria kumkabidhi Mkuu wa Mkoa na hapo hapo nitumie fursa hii kuwaambia watumishi wote na wakuu wa idara kwamba kila mtu akafanye wajibu wake yaani hapa Muheza kuna mauzauza mengi yaani mtu tu akisikia ziara ya kiongozi ikipita anasema uuuuh Alhamdulillah mimi sijagswa kwasabbau anajua angeguswa na yeye asingekuwa salama kwanini sasa tufikie huko, “alisema DC Bulembo.

Katibu wa CCM Wilaya ya Muheza Saimon Leng’ese amempongeza Mkuu wa wilaya hiyo kwa namna alivyoshiriki kuibua matumizi mabaya ya fedha za miradi kwenye Halmashauro hiyo.

“Tunashuhudia mabadiliko makubwa yanayoendelea kufanyika hapa Muheza hata kama ilikuwa ni utamaduni uliozoeleka kule nyima lakini anayabeba na kuyafanyia kazi, “alibainisha Katibu huyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Erasto Muhina na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Emigidius Kasunzu wameelezea mpango mkakati wa usimamizi wa miradi hiyo.

Mwenyekiti Muhina amesema baraza hilo kasi yake kuanzia hivi sasa ni tofauti na kasi ya mabaraza mengine yaliyopita hivyo amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa yale ambayo yanawahusu kwa mujibu wa utaratibu watayasinamia kwa nguvu zote na endapo wakiona kikwazo chochote watakiondoa kwa haraka.

Mhandisi Kasunzu amesema yeye kama mtendaji mkuu wa Halmashauri ameshaandaa timu yake kwajili ya kuhakikisha miradi yote inakamilika kabla ya tarehe 30.

“Ikumbukwe kuwa mheshimiwa Nkuu wa Mkoa alitoa dead line ya miradi hii kukamilika hadi ifakapo tarehe 15 mwezo desemba lakini nimeshaunda timu ya karibu ili kuhakikisha usimamizi ili miradi yote ikamilike kabla ya tarehe 1 mwezi desemba nikiwa na imani kubwa nitapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa watendaji wote, “alisistiza Kasunzu.