December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CRS waadhimisha miaka 60 tangu kuwepo kwake nchini Tanzania

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Shrikila la Relief Services (CRS) ambao ni wakala rasmi wa kimataifa wa kibinadamu wa jumuiya ya kikatoliki nchini Marekani wameendelea kuisaidia jumuiya za kitanzania hasa vijana katika kujiajiri katika masuala afya na kilimo

Shirika hilo pia limeisaidia jumuhiya hizo kwa upande wa lishe kwa kuhakikisha watoto wanapata lishe nzuri, elimu na watu kupata sehemu ya kupata haki zao za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wakiadhimisha miaka 60 tangu kuwepo kwake nchini Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa CRC, Sean Callahan alisema tangu mwaka 1962 CRS imekuwa ikihudumia jumuiya za Kitanzania kwa kujikita zaidi kupunguza umasikini na kutoa msaada kwa watu wanaohitaji msaada zaidi ya 100.

“Wakati CRS duniani inatimiza miaka80, ni heshima kubwa kuwapo Tanzaniakwamiaka 60, tukifanya kazi bega kwa bega na Kanisa Katoliki, washirika wetuwa maendeleona jumuiya tunazohudumia, na kazi hii inaendeleakuwa jukumu kubwakwetukutokana na uaminifu tuliopewa.” alisema callahan.

Aliongeza kuwa CRS imekuwa ikiunga mkono mabadiliko yanayochochewa na jamii kwa kiwango
kikubwa nchini kwa kufanya kazi bega kwa bega na viongozi wa dini mbalimbali, washirika wa kitaifa na jamii
mbalimbali katika njia yao ya ustawi na ustahimilivu dhidi ya athari mbaya za changamoto kuu za leo, ikiwa ni
pamoja na masuala ya jinsia, upatikanaji wa masoko na fedha kwa vijana, uhaba wa chakula na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwa upande wake Katibu wa Mkuu wa Baraza la Maskofu Katoliki Tanzania Pardi Charlse kitima aliiomba serikali ya Tanzania kushirikiana na shirika la CRS kwa kuwa karibu kabisa maana wanachohakikisha kuwa huduma zao haziendi kidini zinaenda kumwangalia wanayemlenga kwa mipango yao ya maendeleo.

“Sasa hivi wamechukua maeneo muhimu afya na Kilimo kwaajili ya kuimarisha vijana kujiajiri kwenye sekta ya kilimo, Eneo la Lishe kuhakikisha vijana wanapata lishe nzuri ,eneo la elimu na maeneo mengine muhimu” alisema Pardi Kitima.

Aidha aliwataka Watanzania kujifunza kujitoa kwa kuwahudumia watu wengine kama shirika hilo linavyofanya kwa jumuiya za kitanzania.

Nae Mmoja ya wafanyakazi wa shirika la CRS Mary Mshota alisema wana miradi katika sekta kilimo , maji pamoja na afya makuzi na malezi kwa watoto wadogo, kupunguza udumavu hasa kanda ya kaskazini miradi ya lishe na kusapoti serikali kipindi cha Covid kuhamasisha maswala ya kupata chanjo na kujichanja.

“Kwa upande wa malezi ya watoto CRS tunaangalia zaidi malezi na makuzi kwa mtoto kabla ya kuzaliwa ni jinsi gani wanaweza kuwasiliana na yule mtoto. Kwa kujenga akili ya mtoto kufikiria vizuri na ubongo uweze kufanya kazi vizuri” alisema mary.

Rais wa Catholic Relief Services Sean Callahan (katikati), Matt Davis, Mkurugenzi wa CRS Kanda ya Afrika Mashariki (wa kwanza kushoto) na Kellie Hynes, Mkurugenzi Mkaazi wa CRS nchini (wa kwanza kulia) wakikata keki kusheherekea miaka 60 ya shirika hilo kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 28 Marchi 2023.