December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chuo cha Afya Muhimbili-MUCOHAS Jitathimini, Uwajibikaji na Uongozi, Prof. Makubi

Na Mwandishi wetu

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ameutaka Uongozi wa Chuo cha kati Elimu ya Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUCOHAS) kujitathimini katika uwajibikaji wao na namna ya Uongozi unavyoendesha mambo yake.

Prof. Makubi ameyasema hayo leo wakati alipokitembelea chuo hicho kufuatia malalamiko mbalimbali yanayowasilishwa Wizarani.

Mara baada ya kuongea na watumishi hao Katibu Mkuu huyo akiwataka Viongozi wa chuo pamoja na watumishi wote kujitathimini na kuhakikisha chuo hicho kinaboresha ufundishaji kwa vitendo pamoja na uwajibikaji wa Menejiment hiyo kwa kuwa karibu na watumishi na wanafunzi

Hata hivyo Prof. Makubi amesema amekiweka chini ya uangalizi wa karibu kwa miezi mitatu chuo hicho ambacho ili kuweza kubadilika na kuwajibika ipasavyo ili kuzalisha wanafunzi bora katika kuhudumia afya za Wananchi. Uongozi umetakiwa unatakiwa kuwashirikisha watumishi katika maamuzi yao, madai na kuwasikiliza kwa karibu sana.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi Mtemdaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamad Janabi.