Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online Singida
UZEMBE mkubwa sana uliofanywa na dereva umetajwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida kuwa chanzo cha vifo vya watu 14 waliokuwa wakisafiri na basi dogo aina ya Hiace kutoka jijini Mwanza.
Ajali hiyo imetokea jana Desemba 13, 2020 saa 9:30 alasiri katika Kijiji cha Mkiwa, Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida wakati gari hilo lilipogongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Kahama.
Kamanda wa Polisi mkoani Singida,Sweetbert Njewike, amesema jana kuwa dereva wa basi hilo alilipita gari la mbele yake bila kuwa na tahadhari kisha kugongana na lori hilo.
“Tumekuwa tukisisitiza mara kwa mara madereva kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani. Ili jambo tunalisisitiza mara kwa mara, kwenye ajali hii kuna uzembe mkubwa sana wa dereva wa Hiace, unapita gari mbele bila kuchukua tahadhari, hii ni barabara kuu lazima uone mbele kuna nini,” amesema
More Stories
Samia, Mwinyi wawapa miezi mitatu wawekezaji
Tanzania,Uingereza kushirikiana katika kuendeleza madini Mkakati
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi