December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chama cha Wanasheria Wanawake chafanya Mkutano Mkuu

Bi. Lulu Ng’wanakilala Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) akifungua mkutano Mkuu wa 32 wa Mwaka wa Chama hicho unaofanyika kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam ambapo wanasheria mbalimbali wananwake ambao ni wanachama wa chama hicho wanashiriki.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-DAR ES SALAAM)

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) Bi. Tike Mwambipile akitoa maelezo kwenye mkutano huo kabla ya kumkaribisha Bi. Lulu Ng’wanakilala Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (TAWLA) ili kuzungumza.

Bi. Lulu Ng’wanakilala Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (TAWLA) na Jaji Mstaafu Joaquine De- Melo wakiwa katika mkutano huo.

Dr. Hellen Kijo Bisimba akitoa mada katika mkutano huo umaofanyika kwenyehoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam.

Jaji Mstaafu Joaquine De- Melo ambaye ni mwanachama wa (TAWLA) akitoa nasaha zake kwa wanachama katika mkutano huo.

Dr Gavin Kweka mwanasaikilojia akizungumza na wananchama wa (TAWLA) na kuwapa mada mbalimbali kuhusu msongo wa mawazo unavyoathiri watu wengi katika maisha.

Picha mbalimbali zikiwaonesha wanasheria wanawake ambao ni wanachama wa TAWLA wakifuatilia hoja mbalimbali katika mkutano huo.