Na David John timesmajira online
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuwa kufanyika kwa mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya chakula hapa nchini kunaweza kusababisha kupunguza tatizo la dola ambalo lilikuwepo hapa nchini.
Amesema kuwa hata kwa upande wa vyakula Tanzanaia itaweza kufaidika na hasa kwa Upande wa Dar es Salaam mkoa ambao ni kitovu cha uchumi wa nchi .
Chalamila ametoa kauli hiyo leo septemba 5 ,2023 kwenye viwanja vya kituo cha mikutano ya Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere ambapo Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya chakula Afrika unafanyika .
Amesema kuwa Dar es salaam ndio Kila kitu kwani Kuna wakazi si chini ya milioni tano na ndio kitovu cha masuala mengine yote yanayohusu biashara za kawaida za ndani na nje huku akisema Dar es Salaam itafaidika sana Kutokana na utalii utakaokuwa unafanywa na wageni mbalimbali wa aliokuja kwenye mkutano huo.
Chalamila ameongeza kuwa kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuja kwenye mkutano huo hadi ukumbi wa Mwalimu Nyerere unaonekana ni mdogo na katika hili inapelekea kupata mawazo ya kuongeza kumbi zingine na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameshaliona hilo na mapema sana ukumbi huo utaaza kupanuliwa Ili kukidhi mahitaji makubwa ya matumizi.
Amefafanua kuwa mkutano huo ni miongoni mwa mkutano mkubwa ambao unafanyika katika ukanda huu huku akisema pia kuna mkutano mwingine mkubwa wa shirikisho la michezo Duniani ambao utafanyikia hapa nchini .
Amesema kuwa kupitia mkutano huo ambao unatarajia kufanyika hapa nchini tayari vyumba vimeshaaza kubukiwa na wito wake Kwa wakazi wa Dar es Salaam nikwamba fursa kama hizo haziji mara mbili hivyo wajaribu kutumia fursa hiyo vizuri ili kuweza kupata faida za mkutano huo mkubwa.
Akizungumzia hali ya usalama Chalamila amesema kuwa mkoa wa Dar es salaam uko salama na hali Iko Shwari na Ulinzi uko Kwa asilimia 100 na hakuna mtu yeyote ambaye atapata itilafu katika kuishi kwake hapa Dar es salaam kuazia Leo hadi utakapotamatika mkutano huo.
Kuhusu vijana Amesema kuwa hivi Sasa kilimo sio tena adhabu kama ilivyokuwa huko nyuma hivi Sasa Rais Dkt.Samia ameleta kilimo kama biashara ,fursa ,kilimo ni sayansi hivyo vijana waliomaliza vyuo vikuu na ambao hawajamaliza watumie fursa hiyo vizuri na watende Kwa vitendo na waifutilie kweli kweli ili kuweza Kubadilisha maisha yao.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi