Na Mwandishi Wetu
BAADA ya mikutano mitatu ya uzinduzi wa kampeni wa Jiji la Dar es Salaam (Kanda ya Pwani), na Kanda ya Kaskazini (Arusha, Manyara, Tanga na Kilimanjaro) Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa ratiba mpya kuanzia leo ambapo kitafanya mikutano katika mikoa saba.
Kwa mujibu wa ratiba ya mikutano ya uzinduzi wa kampeni iliyotolewa leo inaonesha kuwa chama hicho leo kitakuwa na mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Furahisha, Kitangili, jijini Mwanza, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
Kesho, Septemba 2, 2020, chama hicho kitafanya mikutano yake kwenye Uwanja wa Lubaga Joshoni, Manispaa ya Shinyanga, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
Septemba 3, 2020, itakuwa ni zamu Uwanja wa Chipukizi, Tabora mjini, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
Septemba 4, 2020, Uwanja wa Uhuru, jijini Dodoma, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo Septemba 5, 2020, chama hicho kitafanya kampeni Uwanja wa Rwandanzovwe, jijini Mbeya, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
Septemba 6, 2020, itakuwa zamu ya Uwanja wa Sabasaba, mjini Mtwara, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
Ratiba hiyo inaonesha kuwa Septemba 7, 2020, mikutan mkutano utafanyika Uwanja wa Gombani, Chakechake, Pemba, kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana. Na baada kitakuwa na mkutano mwingine Uwanja wa Maisara, Unguja, kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 12.00 jioni.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
27 kulipwa kifuta jasho Nkasi
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini awasilisha hati