November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM yasifu mapinduzi na mageuzi makubwa sekta ya afya

Na Mwandishi Wetu,timesmajira, Online

CHAMA Cha Mapinduzi CCM,kimeipongeza serikali kwa kazi kubwa ya kuboresha sekta ya afya nchini kwa namna inavyogusa maisha ya wananchi wake na ustawi wa Taifa.

Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka baada ya kufanya ziara ya kutembelea hospitali ya taifa ya Muhimbili pamoja na taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kutathmini utendaji na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM.

‘’Tumejionea mabadiliko makubwa sana katika sekta ya afya..kwa kweli tulikotoka ni tofauti na hapa tulipo.hapa tulipo ni bora sana Mapinduzi na mageuzi makubwa katika sekta ya afya tunayoyasikia nje na uhalisia ukifika hapa ni tofauti sana kazi kubwa sana imefanyika’’ amesema Shaka.

Amesema kuwa dhamira na utayari wa Rais Samia Suluhu Hassan kutenga fedha katika budjeti ya serikali shilingi bilioni 630 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya Muhimbili inakwenda kuandika historia mpya katika nchi ikizingatiwa hospitali hiyo imekuwa ni kimbilio ndani na nchi za jirani.

‘’Hospitali hii imejengwa mwaka 1905 wakati huo ikihudumia watu 1,100 kwa mwaka na hivi sasa imekuwa ikihudumia wagonjwa 3000 kwa siku lakini miundo mbinu ni chakavu hasa majengo ambayo mengine yamedumu kwa zaidi ya miaka 70 maono ya Rais Samia ni ukombozi mpya katika Sekta afya nchini ’ amesema Shaka

Amesema kuwa uwekezaji mkubwa katika hospitali ya Muhimbili ni kielelezo cha mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya CCM ibara 83 (p) ambapo leo hii huduma za kibingwa na ubobezi zimekuwa zikitolewa nchi na sio nje ya nchi kama ulivyokuwa imezoeleka na kupelekea kupunguza kwa kiasi kikubwa rufaa za nje ya nchi na kupunguza mzigo kwa serikali katika kulipia gharama za matibabu.

Katika hatua nyingine katibu itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka pia alimtembelea na kumjuilia hali mama ambaye watoto wake walifanyiwa upasuaji wa kutenganishwa ambao waliungana.

Katibu Wa (NEC) Itikadi na Uenezi (CCM), Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Amina Amos Mkazi wa Mkoa wa Simiyu,Mama mzazi wa Watoto Pacha Rehema na Neema walio fanyiwa Upasuji wa kuwatenganisha mnamo tarehe 01 Julai 2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar Es Salaam .

‘’Tanzania kwa mara nyingine inaingia katika historia za utabibu bora na bingwa kufanyika katika nchi yetu, katika eneo la Afrika mashariki kufanyika upasuaji huu ni mara ya kwanza na katika Afrika Tanzania inakuwa nchi ya tatu kufanya upasuaji mkubwa kama huu tukitanguliwa na Afrika Kusini na Misri hii inaonesha ni namna gani uwekezaji huu ambao umefanywa kwenye sekta ya afya umeanza kuzaa matunda..Tunampongeza Rais Samia na serikali kwa nia yake ya dhati katika kuboiresha sekta hii ya afya’’ amesema Shaka

Amefafanua kuwa serikali ilikuwa ikitumia Zaidi ya dola za kimarekani millioni 1.6 kwa mwaka kwa ajili ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu kati ya 200 hadi 300, lakini toka kuanza kwa taasisi hiyo  imepunguza mzigo huo kwa serikali kwa kiasi cha asilimia 95.

‘Ndani ya kipindi cha miaka 3 tumeweza kutibu wagonjwa wa moyo 8, 600 ndani na nje, Sasa hapa tujiulize ingechukua miaka mingapi wagonjwa hawa kupata matibabu kama wangekuwa wanapelekwa hakika ukombozi huu ni wakujivunia, niwahakikishie serikali ya CCM itaendelea kuwekeza katika upatikanaji wa vifaa tiba, kuwaendeleza kimasomo wataalamu wetu sambamba na kuendelea kuboresha mazingira bora ya kutolea huduma” amesema Shaka

wakati akitembelea wagonjwa waliyolazwa katika wodi mbalimbali na katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo alikutana na mgonjwa kutoka Rwanda ambaye amemleta mtoto kufanyiwa upasuaji wa moyo.