May 4, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BRELA Kufanya kliniki kwa wafanyabiashara kesho Arusha

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

wakala wa usajili biashara na leseni wanatarajia kufanya kliniki ya masuala ya biashara na leseni kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Arusha pamoja na kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakwamisha kwenye usajili wa biashara na leseni.

kliniki hiyo ambayo itafanyika kesho Golden Rose itaendeshwa na wataalamu kutoka kwa wakala wa usajilj wa biashara na leseni.

Hayo yameleezwa jana jijini.Arusha na Isidore Nkindi ambaye ni mwakilishi wa mtendaji mkuu wa wakala wa usajili wa biashara na leseni wakati akiongea na wafanyabiashara pamoja na wadau wa mazao ya kilimo kwa mkoa Arusha.

Isidore alisema kuwa wafanyabiashara wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi hasa za leseni lakini pia biashara na wameshindwa kupata majibu yao.

Alisema kuwa sasa wakala wa usajili wa biashara na leseni wameamua kufanya kliniki ambayo itaweza kutoa majibu ya changamoto zote ambazo zinawakabili.

”badala ya wafanyabiashara na wadau kutumia gharama kubwa ya kuja kutufuata makao makuu sasa tutahakikisha kuwa tunazitatua hapa hapa tena na elimu juu tutaitoa hivyo basi ni muimu kwa wafanyabiashara wote sasa kujitokeza kwa wingi hapa Golden Rose”alisema

katika hatua nyingine aliwataka wafanyabiashara ambao wanataka kukua Kwa mujibu wa sheria kuhakikisha kuwa wanafuata sheria za wakala wa usajili wa biashara na leseni lakini pia wahakikishe kuwa wanapata elimu sahihi

Naye Agness Mushi akiongea kwa niaba ya wafanyabiashara ambao wamepatiwa mafunzo na wakala wa usajili wa biashara na leseni alisema kuwa wamefanya jambo jema sana katika kuhakikisha kuwa wanakutana na wafanyabiashara kuanzia ngazi ya chini kabisa.

Mushi alisema kuwa hapo awali wafanyabiashara walikuwa walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya uoga na kuogopa jambo ambalo kwa sasa wakala hao wameweza kuwaelewesha.

Alihitimisha kwa kuwataka wafanyabiashara kuweza kupata taarifa sahihi ambazo sasa zitaweza kuwajenga na kuwafanya kufanya kazi zao kwa uhuru mkubwa sana.

Isidore Nkindi akisitiza jambo jana kwenye semina ya wafanyabiashara n wadau wa mazao ya kilimo nje ya nchi