December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BRELA, ARIPO WAWATEMBELEA MAWAKALA DAR

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

Maafisa Waandamizi kutoka Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), kwa kushirikiana na Maafisa Waandamizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),  wamefanya ziara ya kutembelea Mawakala sita (6) wa Tanzania waliopo jijini Dar es Salaam, kuona namna ambavyo  wanasajili alama za biashara, huduma pamoja na kutoa  hataza kwa wafanyabiashara na wavumbuzi wa Tanzania kupitia mfumo unaosimamiwa  na ARIPO na kusikiliza changamoto wanazopitia Mawakala hao pindi wanaposajili kupitia mfumo. 

BRELA inaendelea kuhamasisha wafanyabiashara kusajili Alama za Biashara na Huduma pamoja na kupata Hataza ili kupewe ulinzi wa Kisheria. Mawakala waliotembelewa ni  Bowmans Tanzania, AKP Laws Advocates, FB Attorneys, NexLaw, Lexglobe IP Services na Crystal Associates.

Maafisa Waandamizi kutoka Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),  wakiwa na Mawakala kutoka Kampuni sita (6) za jijini Dar es Salaam, zinazotoa usaidizi wa Usajili wa Alama ya Biashara na Huduma pamoja na utoaji wa Hataza kwa wafanyabiashara na wavumbuzi nchini.