December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BREAKING NEWS: Mbaroni kwa kumdhalilisha mtoto wa miaka 3

Na Suleiman Abeid, Timesmajira, Shinyanga

POLISI mkoani Shinyanga inawashikila watu watatu kwa tuhuma za mkumfanyia ukatili mtoto mdogo na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Akizungumza na Timesmajira mapema leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba amewataja watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa Irene Pima (32) mmiliki wa baa iitwayo Bondeni, Godius Katisha (32) na Oscar Makondo (35) mkazi wa Mtaa wa Mayila wilayani Kahama.

Watuhumiwa wote walikamatwa mwishoni mwa wiki katika Kata ya Mwakitolyo wakituhumiwa kumnywesha pombe aina ya Balimi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu huku wakimrekodi video kwa kutumia simu na kisha kusambaza kwenye mtandao ya Whatsapp jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Alisema watuhumiwa walifanya kitendo hicho aprili 24, mwaka huu saa sita mchana katika baa iitwayo Bondeni iliyopo kijiji cha Nyaligongo, Kata ya Mwakitolyo, wilayani Shinyanga .

Kwa Habari kamili soma Gazeti la Majira…