Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online,Dar
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, amekuwa kiongozi wa kwanza wa kisiasa nchini kujitokeza hadharani na kupata chanjo ya ugonjwa wa corona, ikiwa ni siku moja tangu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo.
Akizungumza jana katika Msikiti wa Mtoro, Ilala jijini Dar es Salaam katika katika Baraza la Eid El Adha, Waziri Mkuu Majaliwa alisema;
“Chanjo hiyo ipo tayari nchini mwananchi yoyote anayetaka kuchanjwa akachanje kwa ajili ya kupata kinga dhidi ya ugonjwa huo.”
Profesa Lipumba amepata chanjo hiyo leo katika Kliniki ya Umoja wa Mataifa Masaki Dar es Salaam. Prof. Lipumba amewaambia waandishi wa habari mara baada ya kupata chanjo hiyo kwamba huu ni wakati muafaka wa wananchi kupata chanjo ili kuwa salama.
More Stories
Wananchi wa Ikuvilo watakiwa kujitokeza kuhakiki taarifa zao
Watanzania wahimizwa kutenda mema
Nani kuwa mrithi wa Kinana CCM?