January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BREAKING: Bunge lathibitisha Ndugai kuachia ngazi

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Kujiuzulu kwa Spika Ndugai kumekuja siku nne tangu ajitokeze kwenye vyombo vya habari na kuomba msamaha kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote kwa ujumla, kwa kauli yake ya kupinga mikopo ambayo Serikali inakopo, huku akidai kwamba ipo siku nchi itapigwa mnada.

Leo Spika Ndugai alimwandikia Katibu Mkuu wa CCM barua ya kujiuzulu. Kupitia barua hiyo, Ndugai alisema;

“Leo Januria 6, 2022 nimeandika barua kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) barua ya kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uamuzi huu ni binafsi na hiari na nimefanya kwa kuzigatia na kujali maslahi mapana zaidi ya Taifa langu, Serikali na CCM.

Pia nakala ya barua yangu hii ya kujiuzulu nimeiwasilisha kwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya hatua stahili kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na sheria nyingi ili kuwezesha mchakatio wa kupata spika mwingine kuanza.

Nachukua nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa wabunge wenzangu, mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan,  Serikali kwa ujumla na wananchi wa jimbo langu la Kongwa na Watanzania wote kwa ushirikiano mkubwa mlionipa katika kipindi chote nilipokuwa Spika wa Bunge letu tukufu.