Na Bakari Lulela ,Timesmajira
BENKI kuu ya Tanzania (BOT) imezitaka Taasisi za huduma ndogo za Fedha kuweza kujisajili kwenye mamlaka za TAMFI na TAMIU katika usimamizi wa Utoaji wa Mikopo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Emanuel Tutuba amesema kuwa kujisajili kwa Taasisi hizo kutawezesha Mazingira ya Biashara kwenye Taasisi hizo za Mikopo kuimarika na kuepuka kuitwa Majina Mabaya kwa kwa Wananchi.
“Hapo awali Taasisi hizi za Mikopo zilikuwa zikiitwa Majina Mabaya ikiwemo Mikopo Umiza, Mikopo kaba roho” amesema Gavana wa Benki kuu Emanuel Tutuba.
Gavana Tutuba aliongeza kuwa katika kuhakikisha Sekta ya Fedha inaimarika tayari Benki kuu imeweza kusajili Taasisi zinazotoa Mikopo takribani 2600 kote Nchini.
Alisisitiza kuwa Lengo la Benki kuu ya Tanzania BOT ni kuhakikisha Taasisi zitoazo Mikopo zinatoa huduma kwa ubora wa kipekee..
“Unaleta malamiko kwa Gavana usiporidhika na huduma itolewayo na taasisi za Mikopo”Alibainisha Gavana Emanuel Tutuba.

kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Microfinance Association (TAMFI)Devota Minzi ameishukuru Benki kuu ya Tanzania BOT kuungana na Taasisi hiyo ilikuwawezesha Wananchi kupata huduma bora za Mikopo.
Alisema Taasisi hiyo itaendelea kufuata kanuni na Sheria zilizotolewa na Benki kuu (BOT).

“Bado tuna Changamoto za uwezeshwaji hivyo tunaiomba BOT itushike mkono ikiwemo uwezeshwaji kiuchumi”amesema Mwenyekiti wa TAMFI Devota Minzi.
Minzi Aliongeza kuwa Ni vyema Benki kuu ikatoa Ushirkiano ili kuweza kuwafikia walengwa
“Sasahivi tunaitwa Mikopo mitakatifu na sio Umiza”alisisitiza Devota Minzi.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Association of Microfinance institution (TAMIU)Juma Munanka amesema kuwa Taasisi hiyo ipo katika kila Wilaya ikiwemo Tandahimba lengo ni kuhakikiasha Mashirikiano yanaimarika na kuhakikisha huduma za kifedha zinaimarika.
“Sisi kwa haya kwetu ni nuru kwa kuhakikisha Mashirikiano haya yanaimarika kati yetu na BOT”amesema l Mwenyekiti wa Taasisi ya TAMIU Juma Munanka.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako