December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bodi ya Kahawa yatambua mchango wa Prof. Kamuzora

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof.Faustin Kamuzora,(katikati), akikabidhiwa na viongozi wa Bodi ya Kahawa mashine ya kisasa ya kutayarisha kinywaji cha kahawa iliyokaangwa na kusagwa (Roasted and Ground) kama alama ya kutambua mchango wake wa kuwahimiza Watanzania kufahamu faida za kiafya na kutumia kahawa tunayoizalisha nchini. Kushoto ni afisa mauzo ya nje, Fatu kubonye na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa, Prof. Jamal Adam.