May 4, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bodaboda Mbeya watoa msaada kwa waathirika wa maporomoko ya udongo Itezi

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

MWENYEKITI wa Bodaboda jijini Mbeya Aliko Fwanda ameongoza viongozi wa kanda saba za Jiji hilo kutoa msaada wa vyakula kwa waathirika wa maporomoko mlima Kawetere yalitokea aprili 14,2024 na kusababisha nyumba ishirini kufunikwa na udongo pamoja na shule ya mchepuo wa kiingereza ya Generation.

Fwanda amesema bodaboda Jiji la Mbeya wako pamoja na waathirika hao kwani ni wateja wao na uwabeba katika shughuli zao za kila siku.

Amesema huu ni msaada wa awali na kama kuna uhitaji wowote wasisite kutoa taarifa ili waweze kuchangia athari hiyo.

Anthony Maliga Mtendaji Itezi Magharibi
Abraham Anyitike Mtendaji Gombe Kaskazini wameupokea msaada huo na kwamba utagawiwa kwa walengwa.

Wamesema misaada yote inayopokelewa uhifadhiwa stoo na baadae kugawiwa waathirika kwa utaratibu maalumu.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Itezi jijini Mbeya Sambwee Shitambala amewashukuru wadau wanaoendelea kutoa misaada na kuwaomba zaidi misaada hiyo ielekezwe kwenye vifaa vya ujenzi kama mabati,saruji,misumari,mbao na vitu vingine kwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa viwanja 21 kwa waathirika ambao nyumba zao zimefunikwa na udongo.

Hivi sasa waathirika waliokuwa kwenye kambi ya muda shule ya msingi Tambuka Reli imevunjwa baada ya Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini kuwatembelea na kawapa pole waathirika na kuwapa msaada kutoka ofisi ya Rais iliyowakilishwa na William Lukuvi na Barozi Rajab Luwavi.