March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bilia:Vyama tisa vimechukua fomu uteuzi wa Ubunge Ilemela

Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ilemela,mkoani Mwanza,Herbert Bilia,amesema hadi jana Agosti 18,2025,ujumla ya vyama 9 vya siasa vimeshachukua fomu za uteuzi kwa ajili ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Bilia,amebainisha hayo Agosti 18,2025,wakati wa utoaji wa fomu za uteuzi kwa mgombea ubunge.

Ambapo amevitaja vyama hivyo kuwa ni Chama Makini , UMD, CCK, AAFP,DP,NLD,Sauti ya Umma, N.R.A na ACT Wazalendo.

Kwa mujibu wa kalenda ya matukio kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2025 zoezi hilo litahitimiswa Agosti 27,2025 .