Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia, Nape Nnauye (katikati) akiteta Jambo na Kaimu Meneja tawi la NMB Wami Paul Nyoni baada ya kupokea Cheti cha shukrani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa mwaaka wa kitaaluma wa wahariri wenye kauli mbiu ya “Sheria ya habari na maendeleo ya vyombo vya habari” unaofanyika mkoani Morogoro. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deudatus Balile na Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Bakari Machumu (kulia kabisa). Benki ya NMB ilishiriki kama mdhamini kwenye mkutano huo unaoendelea hoteli ya Morena, MorogoroWaziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari, Nape Nnauye akimkabithi Kaimu Meneja tawi la NMB Wami Paul Nyoni (kulia) Cheti cha shukrani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa mwaka wa kitaaluma wa wahariri wenye kauli mbiu ya “Sheria ya habari na maendeleo ya vyombo vya habari” unaofanyika mkoani Morogoro. Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deudatus Balile (kushoto) na Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Bakari Machumu (wapili kulia). Benki ya NMB ilishiriki kama mdhamini kwenye mkutano huo unaoendelea hoteli ya Morena, Morogoro.
More Stories
Milioni 299 kutumika kujenga ofisi za kata
Mtanda asisitiza matumizi ya takwimu serikalini
Maofisa Habari watakiwa kuhabarisha taarifa sahihi