Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga
Benki ya NMB imesema kwa mwaka huu imedharimia kusomesha wanafunzi 200 ikiwemo wanafunzi 50 wa vyuo vikuu pamoja na wanafunzi 150 watakaoingia kidato cha tano mwaka huu lengo likiwa ni kusaidia familia zinazoishi kwenye mazingira magumu.
Hayo yamesemwa na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper wakati wa kongamano la mafunzo kwa wafanyabiashara lililoketi Mkoani Tanga la (NMB bussines club).
Alisema lengo la kongamano hilo ni kujengeana uwezo wa namna bora zaidi ya kuendesha biashara zao ikiwa ni pamoja na kupata elimu sahihi kuhusu benki hiyo itakayowasaidia katika biashara zao.
Alisema benki hiyo imejitolea kufanya hivyo kwakuwa inatambua kuwa kuna wazazi ambao wanaishi kwenye mazingira magumu jambo ambalo limekuwa likiwakosesha watoto wao fursa za kupata elimu.
Alisema benki hiyo kwa mwaka huu kupitia mfuko wake wa NMB foundation imeamua kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa elimu ya juu na wale wanaoingia kidato cha tano kwa mwaka huu.
Meneja Prospar alisema wanafunzi wote wanaotoka katika mazingira magumu na wamefaulu vizuri benki hiyo imejitolea kuwapatia ufadhili wa kwenda kusoma bila changamoto yeyote.
“Benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele sana katika kushiriki kwenye mambo mbalimbali ya kimaendeleo hususani yale yaliyoanzishwa na wanajamii wenyewe Nmb kwa mwaka huu peke yake kwa kupitia faida ya mwaka jana tumetenga zaidi ya bilioni 2 kwajili ya kusaidia jamii kama sehemu ya kurudisha fedha kwa jamii, “alisistiza Meneja huyo wa Kanda.
Alibainisha maeneo ambayo wamekuwa wakishiriki kusaidia jamii katika maendeleo kuwa ni pamoja na sekta ya afya, elimu , maji na barabara pamoja na majanga mbalimbali yanayojitokeza.
Hata hivyo benki hiyo ya NMB imedhamieia kutoa mikopo midogo midogo Kwa kupitia simu ya kiganjani bila ya mteja kulazimika kwenda kwenye tawi la benki kusubiri huduma ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa utoaji wa huduma za kidijitali.
Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper aliendelea kuyasema hayo wakati akiongea na wafanyabiashara wa benki (business Club) hiyo mkoani Tanga.
Prosper amesema kuwa huduma hiyo ya mikopo inampa uwezo mteja wa benki hiyo kukopa na kisha kurudi Mkopo wake Kwa gharama ndogo ,huku akijipangia muda maalum wa kufanya rejesho.
“Kwa kutumia Simu yako ya kiganjani Sasa utaweza kukopa fedha kutoka benki bila ya kulazimika kwenda kupanda foleni na Kisha kufanya marejesho “amesema Meneja huyo.
Aidha amesema kuwa benki hiyo imejipanga kutoa huduma zake Kwa njia ya kidijitali Ili kwenda sambamba na Kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia .
“Pamoja na nafasi nzuri tuliyonayo kwa wateja wetu tumeona tuendelee kutoa elimu kwa wateja wetu kwakuwa wao ndio wanaifanya benki yetu kila siku kuwa benki ya kwanza na kuwa benki bora hapa Tanzania, “alisema
Aliongeza kuwa kama mwaka jana benki yetu iliongoza kwa kutengeneza faida ya bilioni 291 na kuwa benki ya kwanza nchini Tanzania.
Nae Mwenyekiti wa NMB business Club mkoa wa Tanga Roberto Mboya amesema kuwa jukwaa hili limeweza kutoa fursa ya kubadilisha uzoefu miongoni mwao na kusaidia kutatua changamoto za kibiashara.
Mboya alisema kuwa benki ya Nmb imekuwa wasikivu wakati wote katika maeneo mbalimbali na kuwataka wafanyabiashara kuitumia kwa uhuru benki hiyo ili waweze kufikia malengo yao waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kujikwamua na umasikini.
Wafanyabiashara katika kongamano hilo wameipongeza benki hiyo ya Nmb na kusema kuwa licha ya kuwapatia elimu kila wakati lakini benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kusaidia mambo mbalimbali katika jamii inayowazunguka jambo ambalo mabenki mengine yanapaswa kuiga.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi