Na Jackline Martin, TimesMajira online
Katika kuunga mkono juhudi za mapambano ya kansa ya shingo ya kizazi kwa Wanawake ‘ Benki ya NBC imeandaa Marathon iitwayo ‘NBC Dodoma Marathon’ yenye lengo la kusaidia Wanawake zaidi ya 20,000 wenye kansa ya shingo ya kizazi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa marathon hiyo ambayo itafanyika Dodoma tarehe 31 July 2022, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi amesema Kila mwaka zinatokea kesi mpya takribani 1200 za ugonjwa huo wa saratani ya shingo ya kizazi;
“Saratani ya shingo ya kizazi inaongoza kwa vifo vitokavyo na saratani kwa Wanawake hapa kwetu Tanzania, takribani kesi 1200 mpya kila mwaka za ugonjwa huu wa saratani ya shingo ya kizazi”
Aidha Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema Inakadiriwa kwamba Kila miaka baada ya mitatu Kuna vifo takribani 700 vinavyotokana na kushindwa kugundua au kuitambua saratani ya shingo ya kizazi vinatokea
Mbali na hayo Sabi amesema Jumla ya Wanawake 9000 wameweza kupimwa na Kati ya hao 550 waligundulika kuwa na saratani hii ya shingo ya kizazi na wakapatiwa matibabu
Pia Sabi amesema wao Kama NBC wanalengo la kuongeza uelewa, kutoa msaada na kuweza kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na saratani ya shingo ya kizazi;
“Saratani ya shingo ya kizazi inazuilika na inatibika, malengo yetu ni kuongea uelewa juu ya saratani kutoa msaada kwa wananchi hasa wale waliopo vijijini, kuongeza idadi ya wale wanaopimwa mapema na kuweza kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na saratani ya shingo ya kizazi na kuongeza idadi ya wale ambao wanapimwa na wanagundulika wanasaratani wanapata matibabu na kupona kabisa”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage amesema katika saratani zinazoongoza nchini ni saratani ya shingo ya kizazi na hii kutokana na maumbile ya Wanawake inawaathiri zaidi Wanawake ambapo asilimia 100 ya wenye ugonjwa wa saratani ya kizazi ni Wanawake hivyo amewashukuru NBC kwa kuchukua jukumu hilo kuwasaidia Wanawake ili kuhakikisha kwamba saratani hiyo wanaitokomeza nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Mawasiliano kutoka Benki ya NBC, Godwin Semuaye amesema katika harakati za kupambana na kansa ya kizazi kupitia marathon hiyo, Wana lengo la kupata milioni 200 kwa mwaka huu ambapo watazipeleka katika hospitali ya ocean road kwaajili ya matibabu ya Wanawake hao wenye kansa ya kizazi;
“Cancer hii inatibika hivyo sisi kazi yetu ni kufanya Kampeni ya kukusanya pesa, kufanya awareness na lengo letu ni kupata milioni 200 mwaka huu ambazo zitasaidia kuwapa ocean road na kutibu”
Mkuu huyo wa Mawasiliano amesema Muitikio wa watu kushiriki kwenye marathon ni mkubwa ambapo kwa miaka miwili wameshapata zaidi ya watu 4000, na mwaka huu wanategemea kupata zaidi ya watu 5000
Mbali na hayo Mkuu huyo wa Mawasiliano amesema Mchango wa serikali ni mkubwa kwasababu wanashirikiana nao Moja kwa Moja katika kuisaidia jamii
Semuye ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushiriki marathon kutokana na uwezo wao wa kiafya na kujitokeza kwa wingi kuisaidia jamii
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM