April 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya NBC yasaini Mkataba wa maridhiano na Wakala wa serikali Mtandao Zanzibar

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesaini Mkataba wa Maradhiano na Wakala wa Serikali Mtandao (egovernment) Zanzibar, kwa ajili ya kuweka mfumo wa ukusanyaji mapato na malipo ya serikali Zanzibar.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba huo jijini Zanzibar leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alisema; “Benki ya NBC inaendelea kuwekeza katika mifumo
ya TEHAMA ili kutoa masuluhisho ya kibenki kwa makundi yote ya wateja. Leo tunajivunia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Zanzibar chini ya ya Rais Hussein Mwinyi, katika kuiboresha sekta ya fedha kwa kuingiza mifumo ya kidigitali ili kuongeza ufanisi hususan katika kuboresha makusanyo ya mapato ya serikali na malipo kwa wadau wake” alisema.

Ushirikiano huu utaiwezesha serikali ya Zanzibar kukusanya mapato kwa wakati na kwa kuwapa wateja urahisi wa kufanya malipo ya Serikali kwa urahisi katika matawi ya Benki ya NBC,
Mawakala, au kupitia huduma kwa njia ya mtandao kupitia simu za mkononi na kwa njia ya mtandao wa intaneti.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa e-GAZ, Said Seif, alisema, “Tunafuraha kushirikiana na Benki ya NBC, moja ya Benki kubwa nchini Tanzania, katika kuweka mfumo wa
kidigitali wa makusanyo na malipo ya Serikali hapa Zanzibar.

Kama wakala uliopewa dhamana ya uwekaji mifumo ya digitali Zanzibar, tuna dhamira ya kuhakikisha kuwa tunashirikiana na wadau wote wenye uwezo katika kufikia kiwango cha juu kidijitali
katika taasisi za umma hapa Zanzibar” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Nd Theobald Sabi na Mkurugenzi wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar Nd Said Seif Said, wakikabidhiana Mikataba ya Maridhiano baada ya benki ya NBC kuingia makubalianona taasisi hiyo kwa ajili ya kuweka mfumo wa ukusanyaji mapato na malipo ya serikali Zanzibar. Hafla hiyo fupi ya utiaji saini ilifanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Airport.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Nd Theobald Sabi (wa pili Kulia) na Mkurugenzi wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar Nd Said Seif Said (wa pili kushoto) wakionyesha Mikataba ya Maridhiano iliyonigiwa baina ya benki hiyo na taasisi ya EGAZ kwa ajili ya kwa ajili ya kuweka mfumo wa ukusanyaji mapato na malipo ya serikali Zanzibar. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa NBC Nd James Meitaron na Bw Haja Lissa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mifumo na Miundombinu ya TEHAMA Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Nd Theobald Sabi (wa pili Kulia) na Mkurugenzi wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar Nd Said Seif Said (wa pili kushoto) wakionyesha Mikataba ya Maridhiano iliyonigiwa baina ya benki hiyo na taasisi ya EGAZ kwa ajili ya kwa ajili ya kuweka mfumo wa ukusanyaji mapato na malipo ya serikali Zanzibar. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya NBC Nd Godwin Semunye pamoja na Skina Salim Afisa Habari wa EGAZ.