November 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya KCB yazidi kuwainua wajasiriamali kiuchumi

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

NAIBU Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi,amezitaka Halmashauri zote nchini ambazo hazijatoa mikopo kwa wanawake na watu wenye ulemavu kuhakikisha wanatoa fedha hizo ili zikawainue wanawake nchini.

Katambi aliyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati maazimisho ya miaka sita ya kuanzishwa kwa Vikoba Nchini,Maazimisho hayo yamedhaminiwa na Benki ya KCB.

Alisema nia ya Serikali ya awamu ya sita ni kuhakisha inawainua wajasiliamari nchini na kuzielezekeza halmashauri zote kuhakikisha wanatoa kwa wakati baada kubainika bado zipo baadhi ya halmashauri zinachelewa kutoa fedha hizo

Aidha,Katambi alowataka wajasiliamari kushirikiana kwa kuunda vikundi ambavyo vitakuwa na watu waaminifu ili waweze kupata fedha ambazo zinazotolewa na halmashauri baada ya kubainika kukosekana uaminifu kwa baadhi ya vikundi pindi wanapopata fedha hizo kutokomea nazo.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Islam Benk kutoka benk ya KCB ,Amoor Muro,amapo Benk hiyo ni wadhamini katika sherehe hizo,alisema kwa sasa benki hiyo imeweka mazingira rafiki katika kuweza kupata mkopo kwa riba nafuu kwa wajasiliamari waweze kujiajiri wenyewe;

“Tunahuduma za mikopo, uwekezaji, akaunti za hundi lakini pia huduma muhimu kwa vikoba hawa za vikundi ambazo hazina gharama,Kufanya miamala bure bila kulipa gharama yoyote pia wajasiriamali hawa wanaweza kupata mikopo hadi bilioni 2” alisema.