Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Kahama
Serikali wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imetoa ushauri wakulima , wajasiriamali wadodo , wa kati na wakubwa kuchangamkia fursa za uwekezaji unaofanywa na taasisi za fedha wilayani hapa ziweze kuwanufaisha kiuchumi na kujiletea maendeleo.
Ushari huo umetolewa na katibu tawala wa wilaya ya Kahama , Timothi Ndanhya kwenye uzinduzi rasmi wa benki ya EQUITY tawi la Kahama na kuwataka watu hao kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotolewa na taasisi za fedha , mabenki katika kujiletea maendeleo.
Ndanhya alisema wilaya ya Kahama ina bahati ya kuwepo na taasisi nyingi za kifeza kwa kuwa na matawi 12 ya benki yaliyofunguliwa katika wilaya ya Kahama na yamukuwa yakitoa fursa mbalimbali za kiuchumi na kuwataka kuzitumia ziweze kuwasaidia kukuza mitaji yao na kujiletea maendeleo.
Awali katika hotuba yake kaimu mkurugenzi mtendaji wa EQUITY benki Tanzania, Betty Kwoko alisema benki yao ni biashara katika malengo yake , lengo lake kuu ni kuboresha maisha ya kila Mtanzania kiuchumi na jamii.
Kwoko alisema benki ya EQUITY ni miongoni mwa taasisi bora ya fedha katika kutoa huduma bora kwa wateja wake na kwa wafanyabiashara wadogo , wa kati na wakubwa na kutokana na utafiti wake wilaya ya Kahama yenye halmashauri tatu inamalengo ya kibiashara katika kukuza uchumi wa wananchi wake.
Alisema katika mpango wa mkakati wa Benki ya EQUITY wa miaka mitano wameweka malengo sawa na ya serikali ya wilaya ya Kahama kuhusu biashara ya Madini ya dhahabu , Almasi na kwa upande wa kilimo cha mazao ya Pamba , Tumbaku , Alizeti , Choroko , Degu kuhakikisha wanawasaidia kiuchumi wanaofanya shughuli hizo.
Kwoko alisema katika mpango huo pia wamejumuisha pamoja na wajasiriamali wadogo , wa kati na wakubwa wamewajumisha kwenye vipaumbele vya benki hiyo na kuwataka wananchi kuchangamkia huduma mbalimbali zitakazotolewa pamoja na fursa ya kupata elimu bule ya fedha na uwekezaji wa amana , utuzaji wa fedha na mikopo nafuu kwa ujasiriamali mdogo , wa kati na mkubwa.
Nao wananchi na wateja waliofika kwenye uzinduzi huo John Manjale na Delfine Kalunde walipongeza mpango mkakati wa benki hiyo katika kuwasaidia watu wa kada zote za kiuchumi ziweze kuwasaidia  kubadilisha maisha na kujiletea maendeleo.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini