Na Godfrey Ismail
WASHINGTON, Ripoti mpya ya Benki ya Dunia imebainisha kuwa, ukuaji wa uchumi Kusini mwa Jangwa la Sahara umeathiriwa zaidi na mlipuko wa virusi vya corona (COVID-19) vinavyoendelea kusambaa kwa kasi na huenda ukashuhudiwa anguko kubwa katika ukanda huo wa Afrika.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, uchumi huo unatabiriwa kuanguka zaidi kutoka asilimia 2.4 ya mwaka 2019 hadi asilimia -2.1 na -5.1 ndani ya mwaka huu (2020). Benki ya Dunia imebainisha kupitia ripoti hiyo ya ‘Pulse of Africa’ ambao ni mrejeo wa miaka miwili ya ukuaji wa uchumi katika ukanda huo kuwa, kushuka kwa hali hiyo ya kiuchumi itashuhudiwa kwa mara ya kwanza tangu miaka 25 iliyopita.
“Janga la COVID-19 linajaribu mipaka ya jamii na uchumi kote ulimwenguni, na nchi za Afrika zinaweza kukabiliwa na hali ngumu sana.
“Tunakusanya raslimali zote zinazowezekana kusaidia nchi kukidhi mahitaji ya haraka ya watu na maisha wakati pia tunalinda njia za kuishi na kazi kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na wito wa kusimamia kwa malipo rasmi ya huduma ya deni ya nchi ambayo inaweza kutoa fedha kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya afya kushughulikia COVID-19 na kuokoa maisha, nyanja za usalama wa kijamii ili kuokoa maisha na kusaidia wafanyikazi waliopoteza kazi, msaada kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, na usalama wa chakula,”amesema Hafez Ghanem ambaye ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia barani Afrika.
Ripoti kamili jipatie nakala yako ya Majira…
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya