May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Barabara ya kibada-mwasonga -Kimbiji kujengwa kwa kiwango cha lami

Mwandishi wetu, Timesmajira Online, Dar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ameridhia kuongezwa kwa ujenzi wa kilometa 10 katika barabara ya Kibada – Mwasonga – Kimbiji kwa kuunganisha na kipande kilichobakia cha Kimbiji hadi Cheka kwa kiwango cha lami.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam Aprili 29, 2024 na Waziri wa Ujenzi, Inocent Bashungwa katika ziara yake kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua.

“Rais wetu baada kumpelekea taarifa ya changamoto ya barabara hii awali iliyoridhiwa ni kujengwa kwa kilomita 41,Rais ameongeza ujenzi huo uwe wa kilomita 51,” amesema

Alisema tayari Serikali imeshampata Mkandarasi na kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kibada – Mwasonga – Kimbiji yenye urefu wa kilometa 41 kwa kiwango cha lami.

“Hatua iliyopo kwa sasa ni mkandarasi kupeleka mitambo ili mvua zitakapoisha aande ujenzi wa barabara hiyo mara moja kwa kiwango cha lami Kwa kilometa 41 tena bali 51 kwani tunaiunganisha na kipande kilichobakia cha Cheka hadi Kimbiji”, amesema Bashungwa.

Akizumngumzia mji wa Kigamboni amesema muhimu kwa sababu ni wa kibiashara na unatoa mchango mkubwa hivyo aliwataka wananchi wa Kigamboni kutambua mvua zikiacha watajenga barabara zaa kudumu.

Amesema Serikali imejipanga kufanya tathmini kuwa mvua zitakapoisha kurudisha miundombinu ya barabara ya kudumu hivyo hakuna miundombinu itakayoharibiwa na mvua isirudishwe mawasiliano yake.

” Nimekuja kufanya ukaguzi wa barabara zilizoharibiwa na mvua na kurudisha zoezi la uriudishaji wa mawasiliano ya muda ili kuwezesha shughuli za uzalishaji uchumi kuemndelea na mvua zikiisha tutaendelea na matengenezo ya kudumu ya miundombinu hii.

” Hakuna barabara yoyote itakayokatika mawasiliano serikali ikashindwa kuyarejesha kwa sababu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameiwezesha Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa ajili ya kurudisha miundombinu iliyoharibiwa na mvua,” amesema

Pia amesema maeneo yoyote yenye mikwamo serikali iatawapeleka wakandarasi kurekebisha kwa haraka iwezekanavayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema Dar es Salaam ni moja ya mikoa ambayo ilipata athari za mvua hivyo wanatarajia kuufumua ili upitike.

“Dar es Salaam hakuna mafuriko zaidi ya kuziba njia za maji na Dar es Salaam inahitaji kufumuliwa pya kwani inayo mifumo ya maji ya mvua,” amesema

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile amesema changamoto kubwa Kigamboni ni mifereji ya maji hivyo aliwaomba wanaowekeza kwenye barabara waangalie tatizo hilo.
Alisema siku ya Jumatano timu ya Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) itafika Kigamboni
kwa ajili ya kuangalia maeneo yenye changamoto ya maji.