April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bara la Afrika kila mwaka wagonjwa wa TB huongezeka

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

IMEELEZWA kuwa ugonjwa wa TB kila mwaka mamilioni ya wagonjwa wapya wa huo ,uongezeka inayoambatana na changamoto ya huduma za afya ,na Rasilimali duni.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya madhimisho ya kifua kikuu Duniani inayoadhimishwa kila mwaka machi 24 Mkurugenzi wa HDT ambaye ni Mwenyekiti wa Action AFRIKA , Dkt.Peter Bujara, alisema kuwa kuendelea kuwepo kwa vikwazo vya kiuchumi na kijamii kunapelekea madhara makubwa ya yanayoambatana na kuongezeka kwa ugonjwa huo.

Mwenyekiti wa Action AFRIKA Dkt.Peter Bujara alisema sehemu za afya ugonjwa wa TB umekuwa ugonjwa wa 9 katika orodha ya magonjwa Duniani katika kusababisha vifo vingi zaidi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

“Bara la Afrika kila mwaka wagonjwa wa TB uongezeka kutokana na changamoto ya huduma za afya na rasilimali duni,mwaka 2022 watu milioni 2.5 waliugua TB Bara la Afrika ikiwa sawa na robo ya wagonjwa wote wapya wa TB Duniani ” alisema Dkt.Bujara.

Dkt.Peter Bujara ,alisema ilikadiriwa watu 42,4,000 walikufa kutokana na ugonjwa wa TB Bara la Afrika mwaka huo hivyo asilimia 33 ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa TB Duniani vinatokea Bara la Afrika.

Aidha alisema nchi 25 barani Afrika zenye Maambukizi makubwa ya TB baadhi yake ni Angola,Botswana,Cameroon,Congo,Somalia,Ethiopia,Cabon,Guinea Bissau,Guinea Sierra Leone Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uganda, Kenya,Afrika Kusini, Namibia,Zambia,Malawi,na Liberia.

Alisema katika mikakati ya Kidunia ya kukabiriana na ugonjwa huo Mkutano Mkuu wa nchi wanachama za umoja mataifa United Nations High level Meeting _UN HLM on TB) katika agenda ya kukabiriana na TB mwaka 2023 nchi wanachama wa umoja huo waliweka malengo thabiti ya kutokemeza ugonjwa huo ikiratibiwa na Muungano wa wadau dhidi ya TB Duniani yenye makao makuu yake Geneva (The Stop Partnership Global)